“Hakuna sababu za msingi za kulalama juu ya Ali Kiba” Sehemu ya II

Soma sehemu ya 1 hapa chini

“Hakuna sababu za msingi za kulalama juu ya Ali Kiba” Sehemu ya I

Sehemu ya II hii hapa chini.

“Hakuna sababu za msingi za kulalama juu ya Ali Kiba” Sehemu ya II

. Lakini umaarufu wake aliupata kupitia wimbo wake wa Aisha. Hakika umaarufu wake ni mkubwa na hadi leo dunia bado inaburudika na wimbo huo.

Ni wazi ipo mifano mingi ya juu ya wasanii ambao waliweza kufanikiwa kuiteka dunia juu ya sanaa zao za muziki bila kushirikiana na msanii yoyote yule. Isipokuwa jambo la kusimamia ni aina ya muziki unaofanya uwe ni muziki uliojitosheleza.

Hivyo hakuna sababu za msingi juu ya mashabiki kulalama kuwa Ali Kiba ashirikiane na msanii ili aweze kwenda kimataifa. Msanii kwenda kimataifa sio kushirikiana na msanii wa nchi hiyo, wakati wanalaumu wanashindwa kukumbuka njia ya kupromote katika mtandao juu ya kazi ya msanii tena kwa kuchagua nchi atakayo.

Kwa kutumia vyema mtandao kama Youtube msanii anaweza akafahamika nchi yoyote atakayo mara tu kama ataamua kutumia njia ya kutangaza kazi yake kupitia mtandao huo.

Gsy ni msanii ambaye ameweza kujulikana duniani kote kupitia mtandao wa youtube. Msanii huyu amejulikana zaidi na wimbo wake wa Gangnam Style. Na mpaka sasa huu ndiyo wimbo ambao unaongoza kwa kuwa na watazamaji wengi duniani.

Hivyo msanii huyu amefanikiwa bila ya kufanya kazi na msanii mwingine yoyote yule. Hivyo tunaamini kila msanii ana mikakati yake katika kuweza kufikia lengo lake, hivyo hakuna sababu ya mashabiki na wachambuzi chipukizi ambao wanaendelea kujifunza kuendelea kutupa lawama kwa Ali Kiba kwa maana hakuna ajuaye mikakati yake.

Lakini wahenga walisema “Kukosoa jambo usilolijua hata kama umepatia umekosea” Ni ngumu kwa kizazi hiki kuelewa hekima hizi, lakini pia “Huwezi kuona msitu, ukiwa msituni”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa

Mwisho.