“Hakuna sababu za msingi za kulalama juu ya Ali Kiba” Sehemu ya I

“Hakuna sababu za msingi za kulalama juu ya Ali Kiba” Sehemu ya I

Upepo wa lawama kutoka kwa mashabiki lakini hata wale ambao hujivika uchambuzi ilihali hawana hoja ya ujuzi juu ya ujuaji wa muziki namna unavyokwenda wameendelea kulalama juu ya Ali Kiba. Lawana zao kubwa ni kutaka Ali Kiba kufanya kazi na wasanii wa nchi nyingine kwa wingi na kasi kubwa kama ambayo wengine wanafanya.

Ila jambo la kufanya kazi na wasanii wa nje sio baya ni jambo jema kwa namna ya kutaka kufahamika katika nchi husika ya msanii husika ambaye atakuwa amefanyanae kazi hiyo.

Ila pia mashabiki wanapaswa kujua si lazima ufanye kazi na msanii wa nchi Fulani ili uweze kujulikana katika nchi hiyo au kujulikana kimataifa. Isipokuwa huu ni upepo uliovuma Zaidi katika muziki wetu kuwa huwezi bila kushirikiana na msanii fulani wa nchi fulani.

Ipo mifano ya wasanii wengi ambao wameweza kufahamika duniani bila hata kushirikiana na wasanii wa nchi yoyote bali muziki wake kuwa mzuri na wenye vionjo vya upekee venye kuvutia.

Agolo ni wimbo ambao umeweza kupata umaarufu duniani kote ambao ni wimbo halali wa Angélique Kidjo ambaye ni msanii toka Benin. Ambaye pia mwanamama huyu aliweza kuchukua tuzo ya Grammy bila kushirikiana na msanii yoyote kutoka Marekani.

Ila yupo msanii ambaye anaitwa Khaled ambaye wimbo wa Aisha uliweza kumpatia umaarufu duniani kote. Khaled ni mzaliwa wa Algeria lakini baadae akahamia nchini Ufaransa. Lakini umaarufu wake aliupata kupitia wimbo wake wa Aisha. Hakika umaarufu wake ni mkubwa na hadi leo dunia bado inaburudika na wimbo huo.

Itaendeleaa………..

Tufuate kwenye mitandao yetu ya kijamii.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa