Hakuna hoja ya msingi ya wasanii kulaumiwa juu ya Sugu.

Hakuna hoja ya msingi  ya wasanii kulaumiwa juu ya Sugu.

Ni vyema kujua tofauti katika tofauti nyingi ambapo ukijua zitakupa tofauti kubwa katikati ya wengi wenye utofauti wa kujua ukweli lakini wenye hoja dhaifu ambao huendeshwa na hisia na si ukweli.

Tumeona kwa namna ambavyo wasanii wakipokea lawama kutoka kwa mashabiki, wanasiasa na watu wengine ambao  hatujui tuwaweke kundi gani kwa maana ya wakati wote hawaeleweki ambacho wanakisimamia.

Lakini lawama zote za watu hawa kwenda kwa wasanii hutolewa kwa lugha kali na si hoja, lakini wasanii wanapaswa kujua “Usigombane na mkwezi, nazi imeliwa na mwezi” (Akili).

Ni wazi hakuna msanii apingaye juu ya harakati za Sugu katika kuukomboa huu muziki katika mengi mabaya, lakini kuwa msanii wa kwanza kudai malipo makubwa juu ya wasanii katika maonyesho, mirabaha na mengine mengi.

Ni vyema watu wajue kutofautisha siasa na muziki. Kwa sasa Sugu ni Mh Mbunge wa Mbeya Mjini na kesi ambayo inamkabili si kesi ambayo imehusisha Sanaa bali mambo ya kisiasa katika uwanja wao wa kazi zao.

Na waswahili wanasema “Ukijua upande huu, upande huu hauujui”. La!hasha ni vyema kusimama katika njia uijuayo.

Ikumbukwe kama angekuwa na kesi ambayo inahusisha Sanaa ndani yake ni wazi hata Tizneez tungefungua vinywa vyetu kama ambavyo Nay wa Mitego tulivyofungua.

Lakini ingekuwa shangazo kwa watu wote na wasanii kukaa kimya juu ya msanii ambaye angelikuwa anashikiliwa juu ya Sanaa yake ya muziki.

Ni vyema mtafakari haya ya waswahili ya “Ni jambo lipi lisilo na nduguye na mwamu wake!!”

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa