Hakika wengi hawajui ‘kujua kuwa’ na ‘kujua jinsi’ kwenye muziki.

Hakika wengi hawajui ‘kujua kuwa’ na ‘kujua jinsi’ kwenye muziki.

Nyakati hizi wengi katika muziki hasa mashabiki na ambao wamejivika uchambuzi hawajui kuwa wala jinsi.

Maana mchanganyo ni mkubwa mno katika kutoa chambuzi lakini maoni.

Nyakati hizi ili msanii aonekane bora au wimbo wake bora basi ni lazima atoe wimbo kila nyakati ilihali wimbo huo uende na upepo ulipo ‘Trend’ (Fedheha)

Lakini katika wajuzi wa muziki hakika hakuna kipengele cha kutoa nyimbo nyingi kwa nyakati moja ndiyo uwe bora.

Wimbo bora na msanii bora ni kulingana na ubora wa kazi aliyonayo na kazi kudumu kwa nyakati tosha katika sikio la msikilizaji.

Changamoto iliyopo kwenye muziki kwa sasa kwa upande wa mashabiki na wachambuzi ni ‘Kujua kuwa’ na ‘Kujua jinsi’

Na wengi hawapendi kweli, bali uongo mtamu wenye chuki za kishabiki usio na maana wala faida bali ufahari wa lugha kali. Lakini semi kuu ya mswahili yanena “Fahari mama wa ujinga”

Hivyo sisi ni wale ambao hatushangazwi na lugha kali na ujinga wa kiasi cha juu, lakini hufedheheka tu kwa namna ya mashabiki wengi wakiwa hawana maarifa ya kujua kuwa na jinsi.

Na kama wangejua jinsi hakika kungekuwa hakuna shangazo la kushangaa msanii akienda tofauti na upepo uliopo.

Maana ndivyo ambavyo yapasa iwe katika utofauti wa tofauti katika biashara yoyote ile ila hapa ni katika muziki, kwa maana muziki ni sanaa pana mno.

Lakini kama wakijua kuwa muziki ni hisia za ndani za msanii basi pia kusingekuwepo lawama wala lugha kali kwa msanii pale aendapo vyema na upepo wa hisia zake, na si upepo wa muziki uliopo kwa nyakati hizo.

Ila kama wakijua kuwa muziki ni biashara pana hivyo kuna jinsi ya kupanga namna ya msanii kuuza biashara yake basi kusingekuwepo na nguvu ya kutaka fulani afanye kama fulani.

Na hii ni kulingana na kuwa yeye lakini jinsi yeye apangavyo biashara yake ya muziki.

Hakika ni vyema kujua kuwa lakini kujua jinsi, Na mswahili hakucha kusema yakuwa ‘Uzuri wa godoro ndani mna pamba” Tafakari…

#TuzungumzeMuziki