Hakika vitabu vya Mungu ndiyo ufunuo, ilihali vya mzungu vitakuvua nguo” (Nandy na Billnass)

Hakika vitabu vya Mungu ndiyo ufunuo, ilihali vya mzungu vitakuvua nguo” (Nandy na Billnass)

Lakini ni ya kheri ukose vyote lakini si ufahamu, kwa uhalisi wenye halisia.

Kufikiri kabla ya kutenda ni vyema zaidi, maana majuto ni mjukuu.

Wapo wasemao fedheha hii ya Nandy na BillNass kujionesha wakiwa katika faragha itawapandisha kimuziki. (Uongo)

Lakini twasema katika kweli fedheha hii haiwezi kuwapandisha kimuziki bali kuwashusha. Ila kuwatesa katika maisha yao yote ya sanaa lakini nje sanaa. (Kweli)

Lakini fedheha hii itafanya kupoteza zaidi hata ubalozi wa kampuni au kutotumiwa na kampuni. (Uhakika)

Maana hakuna kampuni itakayo balozi mwenye fedheha maana atafadhaisha wateja wao lakini kampuni husika. (Uhalisia)

Nyakati zote mswahili hunena yakuwa “Umaarufu huambatana na upumbavu” na hii imedhirika sasa. (Nyakati)

Tukiwaza kwa sauti ya juu Hivi walijirekodi ili iweje? wafanyie nini? na iwasaidie nini? katika wakati upi?

Lakini kwa utashi mdogo wao hawataacha kupeana lawama katika msambazaji wa video ile, ilhali wanapaswa kujua wao ndiyo chanzo kikuu.
Na uhalisi ule utakaa maisha yote kwenye dunia ya mtandao.

Lakini yapasa tusishangae haya maana mswahili hakuacha kunena yakuwa “Mtembea peku hapendi ila hana viatu” (Ufahamu)

Sis hatuwezi kuweka video ile maana tutakuwa ni wenye kuleta muendelezo wa fedheha juu yao, lakini hata kuendelea kuifedhehesha sanaa kwa ujumla.

Hakika Nandy na Billnass ni mfano wa chemchemi iliyochafuka, Na kisima kilichokanyagwa, hakika hawana maana mbele ya jamii yenye uelewa wa maana ya msanii na sanaa.

#TuzungumzeMuziki