“Grace Matata ni jiwe la msingi lisilopewa thamani stahiki”

“Grace Matata ni jiwe la msingi lisilopewa thamani stahiki”

Wapumbavu wachache watanena muziki wake sio wa Media, swali muziki wa Media ni upi?

Au wangine hunena muziki wake sio biashara, hivi muziki wa biashara ni upi? Jamani katika uhalisi hakuna muziki usiokuwa biashara katika dunia yote. Bali biashara inahitaji matangazo ya kila wakati.

Huoni wapo wasanii ambao wamekuwa biashara lakini katika uhalisi hawana nguvu ya vipaji?, isipokuwa matangazo.

Ni vyema kujua ukubwa wa kipawa cha Grace Matata maana katika kweli katika kizazi cha wasanii hawa wa kike wa sasa tunaowasikia ni wazi hawafikii hata robo ya uwezo wa Grace Matata. Lakini Grace atatoka vipi? wakati wote wadau ndiyo wamiliki wa wasanii wabovu?

Ni wazi yapasa mashabiki muwe wafuatiliaji zaidi katika mitandao na kurasa za msanii husika ili kujua uhalisi.

Tunasema mara nyingi juu ya Grace Matata maana tunaamini nafasi yake ya kipaji ni yapasa itazamwe na watu wengi zaidi. Lakini ni vyema dada yetu utumie mtandao kupromote kwa ukubwa ili ufikie wengi.
Maana ni wazi mdau amejaa hofu na uhalisia lakini ukubwa wa sanaa yako ya muziki. Katika kweli Grace Matata ni bora wa wakati wote kwa wajuzi wa muziki.

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa