Godzillah ni chemchem muhimu iliyochafuka kwa nyakati chache.

Godzillah ni chemchem muhimu iliyochafuka kwa nyakati chache.

“Lawama ya wazi ni kheri kuliko upendo uliositirika” hakika neno kuu lanena kweli hiyo yenye kweli. (Hakika)

Katika simamio kuu la neno kuu hatuwezi kuacha kumpa lawama Zizi. Maana akaaye na kweli na asiinene ni mithili ya mtu mpuuzi, vivyo hatuko tayari kuwa sehemu ya mtu mpuuzi. (Naam)

Lakini ikumbukwe yakuwa  “Upino katika jazo la Godzillah juu ya mitambao katika chezo la maneno hakika ni la juu kupita kiasi” Ilihali mtindo wa mitindo huru huleta ladha katika furahio la mashabiki wengi. (Ndiyo)

Anzo la Godzilla katika uwanja muziki lilikuwa katika upepo mkali ambao kwa hali yoyote ni lazimi usikie/uhisi upepo huo kwa hali ya juu. (Chanzo)

Endelezo lake ni katika punguzo la kasi ya upepo, hakika ni punguzo. Lakini punguzo hili haiwezi kubadili maana ya ubora wa Zillah hata kwa udogo. (Uhalisi)

Tumekuwa watu wa kwanza kabisa katika sikilizo la Masai Land ambao ni wimbo wa Godzillah. (Eeh)

Na daima hupenda mno kujipa muda  katika rudio ili tuelewe vyema muziki. Na katika uwazi  tumeshindwa kuzuia mikono yenye kuandika tafakari juu ya wimbo huu katika chapisho hili. (Kweli)

Pongezi ziende kwa mtayarishaji wa mdundo huu wa Masai Land, dundo lina ujazo imara. Lakini pongezi ziende kwa msanii ambaye amefanya ubeti wa kwanza. (Pongezi)

Soni iende kwa Zizi hakika soni ikujae katika uso wako katika hali ya ukubwa mno. (Soni).  Hatuna hakika kama ameandika mistari ambayo amechana kwenye wimbo huu. (Kabisa)

Ni wazi amekuwa na vina vya kuungaunga kwa uhalisi wa mtu ambaye alikuwa akifanya mitindo huru. 

Kutoa wimbo huu kama rasmi ni kuendelea kujishusha zaidi. Hakika huu sio wimbo ambao Zizi alipaswa kutoa rasmi. (Fedheha)

Zizi anapaswa kutuliza akili mno kwa maana muziki umechangamka kupita kiasi, hivyo kutoa wimbo ambao hauna ujazo kamili wa hadhi yake hakika utampa fedheha tu. (Anguko)

Wimbo wa Masai Land una ugumu mno hata katika lazimisho la kuelewa hata kama ni shabiki kipenzi cha Zizi. (Eeh)

Kujaribu kuupenda wimbo huu ni sawa na ugumu apatae mtu avuapo nguo wakati wa baridi, ama siki juu ya magadi katika onja” (Uhalisia)

Zizi ni chemchem nzuri iliyochafuka na hakika akitulia endelezo lake ni kubwa mno, sisi tunaamini katika Zizi, wimbo huu sio ukomo wa Zizi hata kidogo. (Imani)

#TuzungumzeMuziki