Godzila Anapaswa kujifunza kusoma alama za nyakati.

Godzila Anapaswa kujifunza kusoma alama za nyakati.

Hakika huwezi kutaja majina ya marapa bora kwenye muziki wa kizazi kipya bila kutaja jina la Godzila ambaye ni rapa mzuri aliyechini ya kivuli cha hiphop.

Wimbo kama ‘Get off my way,King zilla,Nataka,Milele,La kuchumpa,na nyingine nyingi ni nyimbo zilizowahi kumuweka pazuri  miaka kadhaa nyuma,2012-2014.

Nani shabiki wa rap muziki na asijue ubora wa Zilla katika kuchezea maneno katika aina yoyote ya mdundo, wakati wowote mahala popote Zila anaweza akafanya chochote katika mdundo ambao utakuwepo. Wengi wamekuwa wakiamini ni mrithi pekee wa marehemu Arbelt Mangweair katika upande wa mitindo huru na kunata na mdundo wowote.

Jambo hili halina ubishi, Zilla ni yuko sawa kote katika upande wa Sanaa ya muziki.

Wapo wapiga miluzi hodari ambao wamekuwa wakimlinganisha Godzilla na Billnas, ingawa mpaka leo sijawahi kujua wanamlinganisha Billnas na Zilla katika upande gani.

Ni jambo la kushangaza tena pale ambapo wapiga miluzi wameamua kuaminisha ujinga wao juu ya walio wengi kuwa Billnas ni mkali kuliko Zilla. Ujinga huu umesambaaa mno, na huwezi kulaumu watu kuamini maana wameshaaminishwa hivyo na wajinga wachache, katika uhalisia unapolinganisha wasanii inabidi utazame mambo mengi ikiwemo,uandishi,midondoko,hata na miaka ambayo wametambulika.

“Akili ya kuambiwa changanya na yakwako”Maana katika nyakati hizi kupata taarifa ni kazi rahisi, ila kupata taarifa/uchambuzi sahihi tena kwa muda sahihi ni jambo gumu, haswa kwa mashabiki ambao huamini kila wanachokisikia kwa wanafiki wenye ushawishi mkubwa wa kupotosha.

Wapo ambao hudiliki kusema Godzilla amepotea kwenye uwanja wa muziki wa rap.Ila katika uhalisia si kweli bali Zilla anajipoteza mwenyewe katika uwanja huu ambao anaumudu kwa aina yake ya midondoko na uandishi.

Licha ya kuwepo kwa nguvu kubwa ya kumpoteza ila Zilla anaweza kuepuka nguvu hiyo katika hali ya kawaida tu bila ya watu wengi wasiojua kuendelea kutokujua ukweli huu unaommaliza Zilla.

Yapasa Zilla ajue “Kioo kinaweza onyesha makosa, lakini kuyasahihisha ni kazi yako”.

Itaendeleaa …

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa