Godzila Anapaswa kujifunza kusoma alama za nyakati. Sehemu ya II

Godzila Anapaswa kujifunza kusoma alama za nyakati. Sehemu ya II

Soma hapa sehemu ya I Godzila Anapaswa kujifunza kusoma alama za nyakati.

Zilla anapaswa kuamka kifikra na kuwaza Zaidi kwanini nyimbo zake tatu hazikufanya vyema ingawa zilikuwa katika ubora stahiki.

Wimbo kama First Class, I get high na Kila wakati ni miongoni mwa nyimbo bora zilitoka mwaka 2016-2017, hakika huwezi kuacha kutaja nyimbo hizi katika nyimbo bora za miaka/mwaka hiyo/hii/huu

Licha ya kuwa bora ila hazikuweza kufanya vyema katika ngazi zote za media.

Nilifikiria Zilla angejifunza kupitia kosa alilofanya katika nyimbo ya First Class na I get High. Ila ameendelea kufanya makosa yale yale, huku wapiga miluzi hodari wakimdanganya kwa siku moja tu ya mahoajino na baada ya hapo si rahisi kumpa muda kama ilivyokuwa awali. Kichekesho ni Zilla kuendelea kung’ang’ana mahala alipo bila kujua uhalisia wa anguko lake kimuziki.

“Ujinga sio kuwa mjinga, bali ujinga ni kuupenda ujinga wenyewe”

Imekuwa ni desturi ya Zilla akitoa wimbo kufanya mahojiano katika vituo viwili tu ama vitatu na kurudi katika mtandao wa twitter/instagram kuandika mambo mengine mengi yasiyo na maana wala faida kwenye uwanja wake wa muziki. Ila Zilla kama Zilla angetumia mitandao hiyo katika kusukuma kazi zake pia ingekuwa ni jambo zuri, ila pia hata kufanya mahojiano katika media nyingine tofauti ukitoa media chache ambazo amekuwa akiishia hapo hakika ingekuwa jambo jingine jema la kuendeleza kusambaza kazi yake.

Nyakati zimebadilika sio zile nyakati za bila fulani hutoki, hivyo Zilla anapaswa kupita katika kila media kama wafanyavyo wasanii wengine ambao wanafanya. (Amewakumbatia wale wale ambao bila wao hutoki)

Kasumba ya kuvimba yapasa imtoke maana haina maana.Si rahisi sasa kwa mtangazaji kuomba mahojiano na msanii kama miaka ya nyuma ya kina Mr II Sugu ila sasa wasanii ndio huomba mahojiano. Hivyo kama Zilla atasubiri mtangazaji amtafute kwaajili ya mahojiano ni wazi ataendelea kubaki pale alipo. Kwa ukubwa wa Zilla hakuna mtangazaji atakaye muomba kufanya mahojiano na mtangazaji akatae. (Muziki umebadilika)

Na tusubiri kuona malalamiko tu ya kusema anabaniwa ilihali ameendela kubaki katika eneo moja, pia ni vyema kuacha kutegemea upande mmoja kwa maana wahenga walisema “Akili tegemezi mara nyingi huangukia ushenzi”

“Kheri ya uvivu wa mwili kuliko uvivu wa kufikiri”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa