Gadner na Jide Vita vya panzi furaha kwa kunguru mweusi

jide

Gadner na Jide Vita vya panzi furaha kwa kunguru mweusi

Ni siku moja kama sio mbili tangu kutokea kwa kusambaa kwa video inayomuonesha mtangazaji Gadner G Habash wa Clouds Fm akiwa jukwaani akizungumza maneno ambayo ni wazi imeonyesha ni udhalilishaji wa kiwango cha juu.

Ikumbukwe Gadner na Lady Jaydee waliwahi kuwa mke na mume, lakini katika mwaka huu imekuwa wazi katika vyombo vya habari kuwa wawili hao wametengana na hawana tena mahusiano kama awali.

Maisha ndivyo yalivyo wakati wote, kutengana katika mahusiano ni jambo la kawaida hasa katika nyakati hizi, ukilinganisha na nyakati za zamani. Ila ni kweli kutengena kwenye mapenzi ni kawaida ila kuna mambo ukifanya hakika haiwezi kuwa kawaida. Moja ya mambo ambayo si ya kawaida ni yale ya kuzungumza mambo ya ndani zaidi kwenye ndoa yenu wakati mkiwa hampo pamoja au mpo pamoja.

Kutazama ya nyuma pia ni jambo muhimu. Kumekuwepo na kuhisi na hata kuibua hoja nyingi katika mitandao ya kijamii mara baada ya kutoka kwa wimbo wa Ndindindi wa msanii Lady Jaydee. Wengi wameonekana kusema eti!Jide amemuimba Mumewe huyo wa zamani. Lakini nilijaribu kuhoji kwenye akili yangu, je ni kweli?lakini pia mbona mara nyingi hizi ndizo nyimbo za Jide?maana hata tangu wapo wote maneno ya kusemwa kuwa anamuimba mumewe yalikuwepo.

Mara zote hupenda kutumia misemo ya zamani ambayo ndani yake inabeba ujumbe wenye maana nzito katika maisha ya leo. Ni wazi jamani vita vya panzi furaha ya kunguru!kwani hatujui?

Hakika hili lipo wazi, ila tabia za watanzania walio wengi ni kupenda kupindisha ukweli ili uongo uonekane ndiyo ukweli. Lakina daima kwenye ukweli uongo hujitenga.

Kiuhalisia kuna vita ambayo sasa inahama na inakwenda kwa watu si tena kama tunavyojua, na hiii vita itakuwa kubwa hivyo tutegemee kusikia mengi kuliko tuliyosikia.

Kumekuwepo na kunguru wawili mweupe na mweusi. Kunguru mweusi ni kunguru ambaye daima amekuwa akiamini hakuna mzoga asiyoweza kuula hata iweje. Na tabia ya kunguru mweusi ni kupenda kuonekana yeye ndiye mwenye haki na mamlaka yote, na kuaminisha watu kuwa hutaweza kuishi kama tu utaamua kumfukuza katika uzio wako.

Ni wazi pia kumeibuka kunguru mweupe ambaye wengi wameanza kuleta imani juu yake na kuona ni wazi haina haja tena ya kuishi na kunguru mweusi ambaye daima tabia yake ni mwenye kuharibu mazao hata vitoweo vilivyokuwa ndani ya uzio.

Nguvu ya kunguru mweupe inapanda kila iitwapo leo, wakati nguvu ya kunguru mweusi imekuwa ikishuka kila iitwapo leo. Maana ni wazi walio wengi wamechoshwa na vurugu za kunguru huyu asiyejali muda wa kula mizoga. Na asiye na aibu mbele za watu maana hata ndani huingia na kuchukua kitoweo atakacho tena mbele ya macho ya watu.

Ni wazi kabisa hasira aliyonayo kunguru mweusi ni kubwa, maana hata watu kuamua kuhama kutoka kwenye uzio wake hii ni wazi haikumpendeza. Lakini ikumbukwe nguvu ya ujanja juu ya kunguru mweusi ni kubwa mno, na akili ya kuvuruga mambo kwenda kama yalivyopangwa anayo.

Kunguru mweupe amekuwa akila mizoga katika utulivu hata watu kupenda kuwa karibu naye, na hata nyakati nyingine kunguru huyu mweupe hupewa vitoweo vilivyo safi kutoka kwa walio wengi.

Wakati kunguru mweusi akiendelea kuamini yeye ni bora zaidi ndani ya uzio, ni wazi tena kunguru mweupe amekuwa akifanya mambo yaliyo bora ndani ya uzio. Hakika huwezi kukataa kuishi na kunguru mweupe, maana ni wazi amekuwa na maisha tofauti na kunguru mweusi na hata kunguru wengine tuliokwisha wasikia na kuwaona miaka kadhaa nyuma.

Ni wazi kitendo cha kunguru mweupe kuamua kushiriki na nguvu ya umma kimekuwa kikimchukiza sana kunguru mweusi, maana ni wazi kunguru mweusi hapendi umfukuze katika uzio wake na uendelee kufurahia maisha bali kuchukua maisha na hata kutaka kumrudisha kunguru mweusi kwenye uzio.

Hili lazima ufahamu, akili ya kunguru mweusi katika kuharibu mambo ndani ya uzio ni kubwa mno, hivyo hata hili lenye kuongelewa sasa katika mitandao ya kijamii ni wazi kunguru mweusi yupo nyuma ya mtu.

Na hakika hapo ndipo furaha ya kunguru mweusi inapoonekana maana nyakati zote hupenda kuona kama umemfukuza katika uzio wake basi uuishi maisha yasiyo na furaha.

Lakini nyakati zimebadilika, wengi wanajua kunguru mweusi alivyokuwa ni kero lakini yeye hujivisha wema ambao kiuhalisia hana hata kidogo. Lakini kwasasa furaha yake imetimia lakini ni vyema kutafakari zaidi, katika hili inamuongezea nini?

Ila pia kuishi na kunguru mweusi yakubidi uwe ni mwenye ufahamu wa kutosha, na pia uwe na akiba ya meneno mana hakuna ajuaye kesho yake.

 

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez