G Nako ni mithili ya Simba dume lenye manyoya mengi shingoni.

G Nako ni mithili ya Simba dume lenye manyoya mengi shingoni.

Hakika mmiliki wa pori katika mbuga ni Simba dume. Ingawaje Simba jike ni mwenye vioja vya mengi katika ukelele lakini si za kutisha mbugani. (Muziki)

Tisho imara ni katika dume na ni kwenye muonekano tu achilia ngurumo lake lenye sauti nzito kiasi na yenye mpangilio kiasi cha kuleta vutio katika sikivu. (Uimbaji/Uchanaji)

Lakini uhalisi wa Simba dume ni utulivu na mambo yake katika ukimya na ngurumo yake, na huwa ni katika uzito wenye tisho imara ambao huleta hamu ya kutaka kusikia kila nyakati. (Kabisa)

Hakuna urahisi wa kumuona Simba dume katika mbuga na hii ni kutokana na uwepo wa wanyama wengi wenye kelele na vurugu za kutosha. (Swala na Nyumbu) Naam (Muziki)

Kumuona Simba dume ni lazima uwe ni mwenye muda mzuri na utulivu kamili si katika mapepe yenye kufuata majani kama swala. (Fikirio)

Hivi yupo ambaye hapendi kusikia sauti ya ngurumo ya G Nako katika nyimbo? Hakika hakuna. (Ndiyo)

Ikumbukwe Simba dume huweka pumziko katika sehemu mosi tu, daima simba dume hana miguu miyepesi katika uzunguko la kutangatanga bali utulivu imara. (Simamio la muziki)

Ni lini umesikia hangaiko za Simba dume (Gnako) katika hangaiko la mengi nje ya muziki? (Hapana)

Hakika muziki wake ndiyo umempa heshima kubwa tangia tangu na tangu mpaka sasa. Na hajawahi kuwa na mepepe wala mbwembwe hata kwa uchache. (Uhalisia)

Ni wazi mbunga umeishika vyema na simamio

la muziki pekee latosha zaidi, na tunapata ujasiri wa kunena hadharani ulionyesha kwenye muziki ni machache kuliko mengi ambayo uko nayo. (Muda)

Katika msitu huu wa muziki wewe ni simba dume na imara licha ya kuwepo kwa kelele nyingi lakini bado imeshindikana zuio la usikivu wa ngurumo lako katika sauti yenye uzito mzuri na imara. (Hakika)

Ikumbukwe hata msitu uweje Simba dume hawezi kushindwa kuishi bali kuishi tena kwa kujiamini. (Naam)

Licha ya hovyo nyingi za kwenye mbuga ya muziki lakini hazijaweza kupoteza usikivu imara wa G Nako kwa watu walio wengi wenye kujua uthamani wa upana wa sanaa. (Ndiyo)

Hakika #TuzungumzeMuziki  G Nako ni mithili ya Simba Dume lenye manyonya mengi shingoni.