Fungeni mageti Billnas na Roma Mkatoliki wanapita.

Fungeni mageti Billnas na Roma Mkatoliki wanapita.

Mdundo unakita kwa uharaka kiasi, lakini ni katika usikivu imara wenye kushawishi kutingisha kichwa kila ala moja inapopiga. (Muziki)

Ikumbukwe muziki ni sanaa inayotumia sauti mbalimbali za kibinadamu na ala za muziki. Na huenda zikawa pamoja au kila mosi na kwa tofauti. (Naam)

Na katika upana wa muziki wapo ambao hupenda mdundo mwingine hupenda mitambao ya msanii, lakini katika upana wa Funga Geti vyote vimekaa usawa wa usawia wake. (Uhalisia)

Billnas si mwepesi katika mitambao yake mithili ya uimbaji lakini upana wa kuchana vyema katika usikivu wa kila sikio lenye kusikia. (Uwezo)

Na katika kweli yenye kweli Billnass amezidi kukomaa vyema kisanaa hasa katika uandishi. Ni wazi mistari yake katika wimbo huu imeonyesha ukubwa wake. (Ukuaji)

Ushiriki wa Roma ni wenye maana kubwa ingawaje wajuzi hawakuwahi hata kuwaza katika uwepo wa kazi moja kati ya Roma na Billnas. (Ndiyo)

Lakini Roma amekaa vyema kwenye mdundo na ameonyesha umuhimu wake katika wimbo huu. (Hakika)

Mr T Touch anakamilisha ujazo kamili wa wimbo huu, hakika ni wimbo wenye ukamili

kwa maana ya mdundo, mistari, mitambao lakini mchanganyo wa wimbo katika ukamilisho wa wimbo. (Naam)

Bila uficho wimbo huu wa Funga Geti ni wimbo wenye ukamili. (Pongezi)

#MuzikiNiSisi