Fid Q Na fasihi za Sanaa zenye utofauti na wasanii wengine wa hiphop.

IMG-20160814-WA0049

Fid Q Na fasihi za Sanaa zenye utofauti na wasanii wengine wa hiphop.

Mtaji mkubwa alionao Fid Q ni uandishi na flow za kipekee, wakati wasanii wengi wa hiphop sasa wakiwa wamejikita kuandika vitu vyepesi imekuwa tofauti kwa Fid Q.

Media zimekuwa zikiwaaminisha wasanii wengi wa hiphop kuwa jamii haiihitaji vitu vigumu, siachi kujiuliza vitu vigumu ni vipi kwenye muziki?. Kwa kauli zao watu wengi wa media hasa Radio na Runinga wamefanikiwa kwa 100% maana sasa wasanii wengi wa hiphop wamekuwa wakiandika vitu vyepesi zaidi.

Nash Mc aliwahi kusema “Mnaandika mapenzi hiyo ni kwa hisani ya Radio Fulani, kwa hisani ya promo mnarudi utumwani” Ni wazi wasanii wengi wanapangiwa cha kufanya. Ila Radio na Runinga zijue kumpangia msanii chakufanya ni kumuwekea mipaka kwenye kipaji chake.

Katika wimbo wa “Sumu” ambao ulitoka Agosti 13 mwaka huu 2016, wimbo huu umeweza kuwa gumzo ndani ya siku chache huku ukiwa umebeba “sumu” za fasihi za Sanaa kwa kiwango kamili.

Fasihi za Sanaa, ni aina ya fasihi inayotungwa kutumia lugha kisanaa, maneno yanayotumiwa katika fasihi huwa ni teule na yenye usanii ndani yake. Utumiaji wa msamiati na miundo ya lugha kwa njia isiyo ya kawaida ili kuibua hisia kama vile, furaha, hasira, huzuni, huruma, n.k. Utumiaji wa lugha ndio huleta tofauti kubwa kati ya lugha ya kifasihi na lugha ya kawaida

Wimbo wa sumu ni wimbo ulitumika kwa lugha nzito ya maneno ya fasihi za Sanaa.

Wimbo wa sumu umebeba maisha halisi ya muziki na nje ya muziki. Ni wazi Fid q amejua anayo haki ya kuongea kama ambavyo ameimba kwenye mstari wa kwanza “Aliyeniumba amenipa mdomo hivyo nina haki ya kuonge”

Ni wazi wasanii wengi wamepigwa kufuri katika midomo yao katika mambo mengi, wamesahau muziki licha ya kuburudisha ila hutumika katika mambo mengi ya ukombozi hasa wa kifikra.

Madawa ya kulevya imekuwa ni kaburi zuri la wasanii wengi wa kizazi kipya, ila mpaka leo wapo wadau ambao hujifanya hawajui kipi ni chanzo cha wasanii wengi kujiigiza katika kaburi hilo. Moja kati ya wasanii wakubwa na wenye heshima aliwahi kusema “Ni msongo wa mawazo na wadau kushindwa kukupa muda hewani huku wakiwa na msanii wao mwingine wakiweza kumtengeneza kuchukua nafasi.

Katika wimbo wa sumu kwenye huo huo ubeti wa kwanza Fid Q amehoji “ Ilikuaje wamuache hadi mshikaji ulaji wa drugs ukamzoea?

Sumu mbele ya wadau wa muziki zimewekwa wazi pale katika ubeti wa kwanza tena ambapo alisema  “ Shibe ya mdau hanilazi njaa sababu Mganga yuko juu, na furaha ya baadhi ya wadau kuona star wanawalamba miguu” Wadau wamekuwa ni watu wa mijivuno na kutaka kuabudiwa na wasanii. Ni wazi kama hujipendekezi kwa mdau ni ngumu kupewa nafasi maana wadau wamekuwa ni watu wasiyo na haya maana upendeleo juu ya wasanii wachache upo wazi.

Ingawa wadau hao hufurahia zaidi msanii ambaye yuko kinyume akianguka kisanii, ila jambo baya ni kwao ni msanii huyo akifanikiwa.

Fid q katika ubeti wa kwanza ameweza kucheza na fasihi za Sanaa katika mlengo wa huzuni, na huruma. Huku kwa upande wake akionyesha jinsi anavyojiamina kwa kusema “Sipigi goti kama Pnc”

Katika ubeti wa mwisho alimaliza kwa kusema “Usipostuka Afrika utazikwa ukiwa hai”

Katika miaka hii Fid Q anabaki kuwa kinara wa muziki wa hiphop, wengi wamekuwa wakiishi kwenye kivuli cha hiphop ila hawafanyi muziki wa hiphop.

Itaendeleaa………

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez