Fid Q na deni la upande wa pili wa mashabiki.

Fid Q na deni la upande wa pili wa mashabiki.

Ni wazi Fid Q ni moja ya wasanii wa ambao hata asipokuwa na wimbo anaendelea kuwepo katika ramani ya muziki wa kizazi kipya. Na hii hutokana na aina ya nyimbo anazofanya lakini uandishi ni jambo jingine linalofanya awepo wakati wote katika vichwa vya wapenda muziki huu.

Sumu na Roho ni nyimbo zake za mwisho kutoka kwake, na ziliweza kufanya vyema katika kila kona ya mashabiki halisi wa muziki wa kizazi kipya.

Utoaji nyimbo nyingi katika muda mfupi kwa upande wa wasanii walio wengi ni mkubwa. Na nyimbo nyingi ni nyimbo ambazo zina maudhui sawa kila mmoja ameimba mapenzi lakini ni katika uandishi mwepesi, na ambao wameimba vitu tofauti ni katika uchache mno. Hivyo bado deni la mashabiki wa aina za nyimbo kama za Fid Q ni kubwa mno.

Lakini wasanii ambao hawajaimba mapenzi ni wachache lakini bado hatujapata ladha bora na safi katika nyimbo hizo, ambazo walau zitatupa muda wakufikiri maana ya neno husika. (Utunzi)

Muziki umepoa kwa aina ya midundo itumikayo na uandishi wake. Hivyo kuna kila sababu ya Fid Q kuja kumaliza deni hili mbele ya mashabiki wenye kiu njema ya kupata ladha tofauti baina ya hizi zilizopo sasa kwa wingi.

“Uwanja huu unamihitaji Fid Q”

#ZimaKikiWashaMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa