Fid Q ataishi katika semi zake katika ahadi kwa mashabiki

Fid Q ataishi katika semi zake katika ahadi kwa mashabiki?

Wajuzi wengi wa muziki wamekuwa wakinena lakini kwa uficho mno yakuwa Fid Q sio mtu wa kuishi katika semi zake.

Ikumbukwe Fid Q ni hodari wa semi nyingi zenye uhalisi wa mengi katika maisha ya wengi kwa kila iitwapo leo.

Tukitoa semi hizo lakini semi kuu katika mwaka huu 2018 ni kutoa album yake ya ‘Kitaa Olojia’ ambapo usibirio wa mashabiki ni mkubwa mno.

Lakini je! ataishi katika semi hii ya utoaji wa album? Maana imekuwa ni zoeo sasa kunena na asitimize.

Lakini hatuachi kumkumbusha kumbukumbu yakuwa “Akusanyaye wakati wa hari ni mwana mwenye hekima, Bali asinziaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha”.

Ni wazi kama asipotoa album ya ‘Kitaa Olojia’ mwezi huu atakuwa ni mwana mwenye kuabisha maana atadhihilisha ni dhahiri si mtu wa kuishi katika semi zake.

Na hizi nyakati za hari kwa pana la ukubwa wake katika nyimbo nyingi ambazo ni wazi ziliweza kushika kwa ukubwa.

Hivyo hili liko juu ya yeye katika kuibeba aibu ya kutotoa album au kuubebeba ushujaa wa kutoa.

Na tegemeo la wajuzi ni kufanya uzinduzi wenye ukubwa kulingana na ukubwa wake, maana haitafaa hata kidogo album hii kutoka kwa uzinduzi wa unyonge.

#TuzungumzeMuziki