FID Q AMEJUA KWENDA NA WAKATI

Fid

FID Q AMEJUA KWENDA NA WAKATI

Huyu na yule ni wimbo uliomtambulisa katika ramani ya muziki wa hiphop nchi Tanzania,miaka ya 2000,na wimbo huu alifanya na msanii Mr Paul, na baadae kufuatiwa na ngoma binti malkia alichofanya na mkali Nuruely na fid q.com aliyofanya na Juma Nature ilifuta baadae tena.

Lakini katika yoye haya msanii Fid q alionyesha umahiri wake katika kile kinachoitwa kunata na mdundo pamoja na mashahiri.

Miaka imeendelea kwenda huku Fid Q akiwa katika msimamo wake ule ule wa hiphop, wakati katika muziki huo umeendelea kuwaacha nje walio wengi akiwemo Madee na hata Mike Tee. Madee aliwahi sema “hiphop haiuzi na anaefanya hiphop ni sawa na muuza pipi”wakati Mike Tee leo amesikika akisema “mashabiki wanapenda nyimbo za kuchezeka”

Licha ya mapema mwaka 2015 Fid Q kusema “kwa kuwa wanajua mshikaji unaishi kwa miiko, na zako itikadi zako zipo kimziki sio kimshiko” Mstari ambao ulionekana umegusa mengi yaliyopo katika soko la muziki wa hiphop maana nyakati hizi watangazaji wengi na wadau pia wamekuwa wakiwakaririsha wasanii et muziki wa hiphop sio wa kibiashara. Kitu ambacho ukitazama kiundani katika muziki wa hiphop si kweli kama haiuzi. Isipokuwa kuna mengi yapo nyuma ya pazia.

Ielewe mitaa ni wimbo wake ambapo ni wazi pia ameonyesha ni jinsi gani ameelewa mitaa na kuelewa sanaa.

Fid Q ni msanii anaejua kwenda na wakati miaka kadhaa nyuma katika game ya hiphop Tanzania kulikuwa muamko wa kufanya wimbo mmoja wasani watatu au zaidi ya watano. Fid Q akadhihirisha hayo katika wimbo wake wa chagua moja alifanya na mkali Adili Chapakazi, Tid, Black Rhino, Langa pamoja na yeye mweyewe Fid Q.

Mapema mwezi huu Mkali ngosha the don au Fid Q ameachia video yake mpya ya Walk off it feat Taz, hakika hii imekata kiu ya mashabiki wake ambao nimepata kuwa nao karibu katika group lao linalokwenda kwa jina la Team Fidq. Mashabiki wengi walikuwa wakitaka video kama hii ambayo amefanya kwa wakati huu.

Ukweli usiojificha ni wazi Fidq amejua kwenda na wakati, nyakati hizi ni zile nyakati za kufanya video kali tofauti na miaka kadhaa iliyopita ambapo wengi hawakuwa wanajali zaidi kuhusu video.

Team tizneez inakupongeza kwa kazi nzuri. Video yake ipo hapa ingia kwenye tab ya music/video utaipata hapo.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez