Fid Q amejua kwenda na wakati kisasa zaidi.

Fid Q amejua kwenda na wakati kisasa zaidi.

Fid Q, Si msanii wa kuongea zaidi bali vitendo vyake husikika kuliko maneno ya wasanii wengi wasiokuwa watekelezaji wa mambo mengi ambayo huwaahidi mashabiki wao na mwisho wa siku hushindwa kutekeleza.

Fid Q huzuka tu na jambo, na huwa linaamana kubwa katika muziki wake. Hata mwaka 2016 alipotoa wimbo wa Walk it off ambao alimshirikisha Taz hakuwa amesema, na wimbo ulikuwa mkubwa kuanzia upande wa audio na video, siachi kusema wimbo huu  kwa mwaka 2016 ni moja kati ya nyimbo bora kuanzia audio mpaka video.

Ikumbukwe wasanii wengi hutanguliza picha na hata video clip wakiwa wana mipango au wanafanya maandalizi ya jambo fulani,sio jambo baya ila kwa Fid Q imekuwa tofauti kabisa, mara zote huonyesha vitendo zaidi.

Katika wimbo wake wa Ielewe Mitaa ambao ulitoka mwaka 2012 alisema” Ukienda mbio na muda mtapishana, mafanikio huja kwa kupenda kile unachofaya”

Ni wazi amekuwa akiishi katika kauli zake na jumbe zenye mafunzo mengi kuanzia kwake na jamii nzima ya wapenda muziki wa hiphop na wengine wengi.

Ni wiki kadhaa tangu amsaini msanii Big Jahman katika Label ya Cheusi Dawa. Ila Big Jahman sio msanii mchanga kama wengi katika kizazi cha mtandao wa picha Instagram kinavyoandika.

Big Jahman yupo tangu miaka ya 2002 ambao alikuwa akifanya kazi na Akili The Brain, Castro na hata marehemu Steve 2k.

Katika mahojiano ambayo amekuwa akifanya katika kumtambulisha Big Jahman pamoja na wimbo wa Mabundi amekuwa akisema “Kwanza nimemsaini Big Jahman maana ni msanii mwenye vision pia uwezo wa kimuziki lakini nidhamu ya kazi”

Fid hakuweza kuficha hisia zake juu ya aina ya muziki wa Ragger Dancehall ambapo alisema “Mimi ni shabiki mzuri tu wa aina hii ya muziki huu ambao anafanya Big Jahman.

“Mafanikio huja kwa kupenda kile unachofanya” Narejea kauli yake hii na kuona maamuzi mazuri ya Fid Q ya kumchagua Big Jahman kuwa katika Label ya Cheusi Dawa, hivyo kwa kuwa Fid Q anapenda aina hii ya muziki tutegemee mafanikio kwake na hata kwa Big Jahman.

Katika swala la Fid Q kumsaini Big Jahman ni wazi amejua kwenda na wakati kisasa zaidi maana upepo wa wasanii kuwa na wasanii wao unavuma vyema. Ila ukimsikiliza Fid Q utajua jinsi ambavyo amejipanga na sio mtu aliyekurupuka na asiyejua anachokifanya.Kwa lugha rahisi sio mfuata upepo.

Kwenda na wakati ni swala ambalo limekuwa likiwaangusha wasanii wengi mno.Kujifunza kwa walio fanikiwa ni jambo jema, kwa uwezo wa kwenda na wakati vizuri katika sanaa ya muziki inapaswa wasani wengi wamtazame Fid Q kama kioo.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez