Fid Q amejichafua kwa wino wa kalamu yake mwenyewe. (Eeh)

Fid Q amejichafua kwa wino wa kalamu yake mwenyewe. (Eeh)

“Achafukaye mfute” na hatuna shida wala hatuna soni kumfuta vyema na kitambaa kaka yetu Fid Q. (Naam) 

Maana haitupendezi kumuona akiwa amechafuka mbele ya macho yetu, kwani kuna ambaye hajui uchafu si kitu chema? (Hakuna)

Kiukweli imekuwa jambo baya na kustaajabisha kwa kaka yetu Fid Q kunena hadharani kuwa sisi ni sehemu ya kumchafua.(Ajabu)

Lakini kama haitoshi kutuita “Washenzi” lakini hatufanikiwa katika kumchafua na hatufi moyo. (Fid Q)

Tukisikiliza tungo zake aandikazo kwenye nyimbo hakika ni wazi ni mtu mwenye kujichafua kwa wino wa kalamu yake. (Kabisa)

Tungo zake ni zenye kufunza na kujenga mengi, lakini mbona hazina uhai ndani yake? (Soni)

Lakini hii inatupa maana yakuwa “Fid Q ni msanii mwenye kupenda kusifiwa zaidi” hataki hata chembe ya kukoselewa. (Chekesho)

Jifunze kupokea yote kwa usawa kwa maana “Ili msanii ufanikiwe inabidi ukoselewe inapobidi usifiwe. (Afande Sele 2002 Watu na Fedha)

Tizneez tumeandika maandiko mengi ya kusifu mengi katika sanaa yako hii, leo kunena hadharani kuwa ni watu ambao ni washenzi ni kutukosea heshima kubwa. (Ndiyo)

Na hatutaki kabisa kuamini yakuwa umeandika bila fikirio bali hasira katika ponda kubwa ya mashabiki juu ya video ya mama yake na Zillah lakini tajo la watu wala rambirambi. (Dhanio)

Lakini yote ya yote tunapenda ujue yakuwa tunaheshimu mno uwepo wako katika uwanja wa muziki. (Hakika)

Vivyo ni vyema ukachunga machapisho katika mtandao maana “Liandikwalo halifutiki” (Naam)

Na kwa hili kaka yetu la kutuita washenzi umepotoka mno na tunapenda ujue yakuwa “Mtu mzima akivuliwa nguo hadharani huchutama” (Nyakati Zote)

Tazama alichoandika kwenye mtandao wa picha ‘Instagram’

 

#MuzikiNiSisi 

Attachment