Fahamu wasanii 3 waliokuwa mbele ya muda, ila anguko lao la sasa linashangaza.

Fahamu wasanii 3 waliokuwa mbele ya muda, ila anguko lao la sasa linashangaza.

Kwa kuwa tumeamua kuzungumza muziki hakuna sababu ya kufunga vinywa vyetu juu ya wasanii ambao kwa namna ya ufanyaji wao Sanaa ya muziki ilikuwa uko mbele ya muda.

Wapo ambao husema muziki umebadilika kwa namna ya wasanii wengi wafanyavyo sasa katika mambo 3 kuanzia flow, swag, na rhymes.

Ni wazi katika vitu hivyo vitatu ni wazi miaka kadhaa nyuma kuna wasanii ambao waliweza kuvifanya ambapo walifanikiwa vyema kwenye sana ila inashanganza leo hii kuona hawasikiki kabisa katika ramani ya muziki wa kizazi kipya.

Team Tizneez tumeona kuna kila sababu ya kuwakumbusha watu yakuwa wapo wasanii watatu ambao waliweza kuufanya muziki wao kwa wakati huo katika muda huu wa mbele katika flow, swag, na rhymes.

Wasanii hawa ni Joslin, Pig Black na Noorah. Kiukweli vipaji hivi vinashangaza kuanguka kisanaa katika miaka hii ambapo muziki umekuwa mwepesi Zaidi.

 

Tuambie msanii gani mwingine unadhani alikuwa mbele ya muda kwa mambo haya matatu yani flow, swag, na rhymes.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa