Fahamu wasanii 10 waliofanya shoo bora ya Tigo Fiesta 2018 Morogoro

Tigo Fiesta 2018 imeanza jana, na Morogoro ndiyo imepata nafasi ya kufungua pazia juu ya tamasha hili ambalo ni kubwa zaidi Tanzania.

Na wasanii shiriki katika jukwaa la Tigo Fiesta jana ni wengi mno, na hii ni desturi ya Fiesta kuchukua wasanii wengi zaidi.

Ila katika wasanii wengi ambao waliweza kupanda kwenye jukwaa hili wasanii ambao wameweza kufanya shoo kwa ujazo kamili ni hawa 10.

Ikumbukwe tukisema ujazo tunaamisha utumbuizaji wenye maana na kumfanya shabiki aseme naam! kweli pesa yake imekwenda kihalali sio kelele za msanii katika tuimbe wote.

Sasa msanii unamuambia shabiki muimbe wote ili iweje? wakati yeye amalipia kuja kuona ambacho unakiimba. Ni vyema shabiki aimbe mwenyewe tu katika raha yake.

Na hawa ndiyo wasanii 10 ambao wamefanya shoo kali zaidi siku ya jana

1. Mr Blue
2. Ben Paul
3. Rostam
4. Country Boy
5. Prof Jay
6. Whozu
7. Bright
8. Mario
9. Maua Sama
10. Fid Q
Zingatia namba tafadhari, na tutakuwa tunaweka listi kila Mkoa ambapo Tigo Fiesta itakuwa ikipita.

#TuzungumzeMuziki