Fahamu msanii wa kwanza wa Hiphop Tanzania kufikisha watazamaji milioni 1 ‘Youtube’

#TizneezThrobackMusic

Fahamu msanii wa kwanza wa Hiphop Tanzania kufikisha watazamaji milioni 1 ‘Youtube’

Wengi hudhani ni mtu wa Kenya lakini hapana Azma Mponda ni mtanzania tena mwenye asili ya Mbeya.

Na ni moja ya wasanii ambao wamekuwa na upepo mzuri Kenya kuliko Tanzania. (Uhalisi)

Na Je! wajua yakuwa Azma ndiye msanii wa kwanza wa Hiphop Tanzania kuwahi kufikisha watazamaji milioni 1 katika mtandao wa ‘Youtube’? Naam! ndiyo ilivyo hivyo na inavyoaminika.

Na wimbo wake wa ‘Jinsi ya kumfikisha mpenzi’ 2014 ndiyo wimbo halisi uliompa watazamaji milioni 1.

Na kwa mujibu wake Azma anasema “Wimbo ulichukua miezi 6 kufikisha watazamaji hao milioni 1. Lakini sikuwahi kufanya promosheni za mtandao hata mara moja”

Na wajuzi hawaachi kunena yakuwa “Kila msanii anao uwezo wa kuweka rekodi nyakati zozote zile za muziki.

Kikubwa na kutengenza kazi yenye ubora wa kuweza kuweka rekodi zenye upekee”
#TuzungumzeMuziki