Fahamu Miaka 17 ya Album ya kwanza Prof Jay katika ubora wa sasa 2018.

Fahamu Miaka 17 ya Album ya kwanza Prof Jay katika ubora wa sasa 2018.

Hakika nyakati zaenda kasi kwa shangazo, maana ilikuwa 2001 juzi tu katika tafakari lakini sasa ni 2018 katika leo.

“Machozi Jasho na Damu” ni album ya kwanza ya Prof Jay ambayo ilitoka mwaka 2001. Na Album hii ni chini ya mikono ya P Majani ndani ya Bongo Records.

Ila album hii ilitoka baada ya album ya Hard Blasterz ambayo yaitwa ‘Funga kazi’ mwaka 2000. Ikumbukwe Prof Jay ni mmoja kati ya waunda kundi la Hbc.

Album hii ya ‘Machazi Jasho na Damu’ ina uhalisi wa uhalisia katika nyakati za sasa katika upana wa yote, yani siasa, muziki, na maisha ya kila leo kwa kila mmoja.

Album hii ni kichwa kilichobeba mengi ambayo yanajenga katika elezo pana la upana wa sanaa na ukubwa wa maana wa Prof Jay.

Wajuzi wanaamini yakuwa hii ni moja ya album bora za nyakati zote katika muziki wa kizazi kipya.

Na album hii ilipambwa na nyimbo kama Ndiyo mzee akiwa na Lady Jaydee na Mc Babu Ayoub, Jina Langu pamoja na Bongo Dar es Salaam akiwa na Lady Jaydee.

Lakini hatuwezi kusahau nyimbo kama Yataka Moyo, Nawakilisha, Piga Makofi, Niamini, Salamu Bibi na Babu, Tathimini akiwa na Jay Mo, Na Bado pamoja na Machozi Jasho na Damu ambapo ndiyo wimbo uliobeba jina la album hii.

Mpaka sasa album hii inatimiza miaka 17 tangu kutoka kwake 2001. Na ubora wa usikivu katika ladha ujumbe uko katika upana mkubwa wa mengi ya sasa.

Hii inaleta maana yakuwa “Muziki pekee ndiyo utaishi” Hivyo msanii wekeza katika muziki kwa upana wake, si katika matendo mengi ya hovyo. Maana hovyo hupita na kukua cha mfadhaiko mbele ya wajuzi.

Naam! daima #TuzungumzeMuziki