Fahamu mfanano wa muziki wa sasa na zamani katika makundi.

Fahamu mfanano wa muziki wa sasa na zamani katika makundi.

Wapo wengi ambao wamekuwa na ulizo kwetu juu ya makundi mengi ya sasa katika wasanii wengi kwenye uwanja wa hiphop. Na wengine huona jambo hili ni jipya kabisa.

Lakini tangu kuuchipuka kwa muziki wa kizazi kipya katika upana wa hiphop kulitawaliwa na upana wa makundi mengi. Jambo la makundi lilikuwa ni ulazima hasa katika nyakati za mashindamo mengi yaliyokuwa yakifanyika.

Yo rap Bonanza 1994 ni mfano halisi ambapo ilikuwa ni lazima ushiriki wa msanii uambatane na kundi si msanii katika hali ya mmoja mmoja.

Katika uwanja wa muziki hakika kulikuwa na makundi mengi mno katika kizazi cha kwanza muziki. Ambapo uwepo wa Weusi Wagumu Asili (WWA) ulileta chachu yake.

Ila hatuwezi kusahau kumbukumbu za Tribe X, Kwanza Unit, Villain Gangstarz, Raiders Posse, Niggaz 2 Public, Gwm, Dar Young Mob, Hard Blasterz, No name, na makundi mengi mengi.

Na hata katika kizazi cha pili cha muziki kwa ujuzi wa wajuzi wananena yakuwa hakukuwa na makundi kwa hali ya upana ila makundi yalikuwepo kwa udogo.

Hivyo wasanii wengi walikuwa na upekee katika kuonyesha uwezo binafsi zaidi. Ingawaje hatuwezi kusahau kundi kama Ghetto Boys, Wanaume Familly, University Corner, East Cost Team, Nako 2 nako, Wachuja Nafaka, na makundi mengine mengi.

Na katika nyakati za sasa tunaona namna ya mfanano wa wasanii kufanya kazi katika upana wa makundi. Kimsingi ni jambo jema kama kuna mlengo wa usawia katika lengo kuu.

Hivyo kwa wale ambao wanaona ni jambo jipya na la ajabu hapana si jambo jipya wala lenye uajabu bali uhalisi wa awali ya muziki.

Na hakika ushindani utakuwepo kwa upana wake kwa kuendelea kuibuka makundi mengine mengi. Kwa sasa tuna makundi kama Rostam, SSK, Moco, Weusi, Sisi the trio, na makundi mengine mengi, hiyo tunatarajia ushindani wa kibiashara zaidi.

#TuzungumzeMuziki