Fahamu mambo mawili yanayomyumbisha Pam D katika muziki wake.

Fahamu mambo mawili yanayomyumbisha Pam D katika muziki wake.

Sisi ni watu wenye imani kubwa na kipaji cha Pam D, na wala hatuna soni kuinena kweli hii mbele za watu.

Ingawa nyakati hizi ni wazi Pam D ameyumba mno katika upande wa muziki ukilinganisha na nyakati za wimbo kama Nimempata na Popo lipopo akiwa na Mesen Selecta.

Na katika mambo mawili ambayo yanamyumbisha kiwepesi ni mtandao lakini neno ‘Mabadiliko ya muziki’.

Kwa wajuzi wa muziki ni wazi hunena yakuwa “wao haawamini katika mabadiliko ya muziki bali muziki ulioko ndani yako”, na hapa wakiwa na maana yakuwa ‘Muziki ni hisia’.

Hivyo usibadilike ukaacha hisia zako na kwenda katika hisia za wengine, hakika hapo utapata anguko.

Mabadiliko ya muziki katika hisia yamemfanya Pam D kuimba wimbo wa singeli ambao ni ‘Umepenya’ akiwa na Msaga Sumu.

Katika kweli si wimbo wa hadhi yake Pam D katika upana wa ubora. Hivyo wimbo huu umepita kiwepesi bila usikivu wa sikio la shabiki, hakika umepita kiwepesi mfano pepo zipepeavyo katika fukwe ya bahari ya hindi.

Lakini mtandao umemuendesha zaidi kiasi cha kuweka video nyingi ambazo si uhalisia wake kwa wengi ambavyo wamezoea.

Ni wazi hii katika wachache kuaminisha wengi yakuwa ya hovyo ndiyo yenye nguvu, na wenyewe siku hizi huita ‘Trend’.

Hakika inabidi mtandao kwenye kurasa zake auendeshe yeye na sisi mtandao kumuendesha, Na wala hapaswi kutazama hizo ‘Trend’ ni vyema kusimama katika njia yake Pam D ambayo mwanzo wake ulikuwa mwema.

Wala asitamani njia za hovyo zaidi bali njia zenye maana ambazo mwanzo zilimpandisha vyema, lakini ni vyema kujua neno kuu lasema “Usiwahusudu watu waovu, wala usitamani kuwa pamoja nao”

Pam D simama katika njia yako ambayo mwanzo ulichonga vyema katika safari yako ya muziki. ‘Usiyumbishwe”

#TuzungumzeMuziki