Fahamu album ya Geez Mabovu na Albert Mangwea baada ya vifo vyao.

Fahamu album ya Geez Mabovu na Albert Mangwea baada ya vifo vyao.

Geez Mabovu na Albert Mangweair Pini wasanii wa hiphop ambao kila mmoja alikuwa na ladha yake yenye upekee.

Ambapo kwasasa wote ni marehemu, hakika “Chenye asili ya kiumbe hakikosi deni la kifo” Naam! kwa nyakati zao wametimiza vyema kama ilivyompendeza Mungu.

Lakini wasanii hawa wote wameacha album zao zikiwa hazijatoka, Album ya Geez Mabovu ipo kwa Lamar (Fish Crab) na ilirekodiwa tangu 2007.

Lakini Albert Mangweair ni katika studio tofauti tofauti, ambapo M To The P amethibitisha hilo pia.

Ngwea alifariki mnamo 25.5.2013 nchini Afrika ya Kusini na kuzikwa kwao Mkoani Morogoro Kihonda.

Wakati Geez Mabovu alifariki 12.11.2014 Mkoani Iringa na maziko yalifanyika Iringa hapo hapo kwa maana ya kwao pia.

Lakini Je! album zao zitatoka lini? katika kweli yenye kweli kiu ya mashabiki ni kubwa katika kusikia wasichowahi kusikia kutoka kwao.

Muda huu ni sahihi zaidi kwa wahusika kuweza kufanya maamuzi mazuri juu utoaji wa nyimbo zao lakini album kwa upana zaidi.

Kwa hakika “Watu watapita isipokuwa muziki” Naam! “Chema hakikai, hakina maisha” ni uhalisia.

Na wapumzike kwa Amani Geez na Albert, mlichoacha kwenye muziki chatosha kumbukuka kumbukumbu zenu nyakati zote.

#TuzungumzeMuziki