Ewe! shabiki ni nani aliyekuroga kiasi cha kushindwa kutafakari juu ya uhalisi?

Hakika “Utu busara, Ujinga hasara” na uhalisi wa wengi wenye vinywa vichafu katika kurasa nyingi za wasanii.

Wengi ni wepesi mno katika kutoa lugha kali juu ya msanii mwingine kutoweka picha mtandaoni pale ambapo msanii mwingine amefariki.

Jambo hili la lugha kali si jema,tukumbuke yakuwa busara ni ushiriki katika yote juu ya marehemu si kuonyesha katika mtandao.

Lakini katika ushiriki pia ni kutokana na nafasi ya msanii husika, na haipaswi kulaumu kwa yoyote kama asipofika wala kuweka posti kwa namna ya uhalisi ulivyo.

Na wakati shabiki ukitumia lugha kali juu ya msanii mwingine je!wewe umetenda yepi juu ya msanii huyo?

Ewe! shabiki ni nani aliyekuroga kiasi cha kushindwa kutafakari juu ya uhalisi?. Haipaswi kumnyooshea mtu kidole, bali anza wewe kwa nafasi yako, hakika yatosha.

Lakini hatupaswi kuwashangaa wenye lugha kali mtandaoni maana hata mswahili anena yakuwa “Samaki huanza kuoza kichwani” ilihali “Uzuri wa godoro, ndani mna pamba”(Fedheha)

Jifunze, Jitafakari, ushabiki sio lugha kali bali hekima ya kunena katika hoja yenye maana.

#TuzungumzeMuziki