Eti! Hiphop haiuzi? una akili wewe?

Eti! Hiphop haiuzi? una akili wewe?

Dunia nzima “Hakuna muziki usiokuwa biashara” na andiko hili tuliandika 2016 katika fafanuzi pana mno. (Hakika)

Hakuna chukizo kwetu kama tukisikia mtu akinena eti hiphop haiuzi? hivi haiuzi wapi? mliwahi kutaka kuuza na ikashindikana? (Ulizo)

Kimsingi biashara yoyote inategemea matangazo mapana ili mlaji aweze kushawishika na bidhaa husika. (Ilivyo)

Sasa kama hamna matangazo katika upana watauza wapi? walaji watajuaje kama bidhaa hiyo husika ipo? (Soni)

Biashara ni matangazo ndiyo maana unaona kuna makampuni tangu tunazaliwa yapo na yanaendelea kwa upana wa matangazo tena kwa gharama kubwa. (Eeh)

Sasa wewe ambaye unasema hiphop haiuzi umeitangaza wapi?. Hivi hamuona mfano wa saa mbovu singeli iliyonena majira yenye kweli? (Uhalisi)

Saa 3 za singeli Efm Radio pekee imetosha kubadilisha nyeusi kuwa nyeupe katika biashara. Tena wakati huo hata wanachoimba sisi huwa hatusikii zaidi ya neno ‘Wauni miluziii’. (Chekesho)

Vivyo basi kama hiphop ikipewa nafasi ni biashara kubwa zaidi, furaha yetu kubwa mno kuona Wasafi Festival inasajili wasimamia misingi hodari wenye kuambiwa hawawezi

kuuza ilihali hawapewi matangazo. (Kabisa)

Stereo na One the Incredible ni safi kuwepo Wasafi Festival hakika mnastahili, maana kiu ya mashabiki kubwa katika muziki wenu. (Naam)

Lakini ndugu zetu wenye Wasafi Festival tunawakumbusha tu kuhusu Maalim Nash Mc hakika anastahili kwa upana mkubwa. (Kumbusho).

Simamio la sanaa imezaliwa upya tunaliona vyema, lakini msije mkakengeuka baada ya kuja kushika usukani. 

Wenzenu pia walianza vyema ila sasa washapoteza uelekeo, mana nao hawana tofauti na wale ambao walikuwa wakiwaponda. (Ajabu)

Eeh! mswahili hakuacha kunena “Shika lingali kichwani” Tafakarini….

#TuzungumzeMuziki