“Enyi wasanii ishini kwenye hekima na busara za Afande Sele”

“Enyi wasanii ishini kwenye hekima na busara za Afande Sele”

Daima ukweli husimama wenyewe bila kujali upo mbele ya nani wala nyuma nani. Lakini ukweli utuweka huru nyakati zote.

Ni wazi wakati wote tumekuwa wakweli mbele ya wasanii wa muziki wa kizazi lakini mashabiki wake.

Lakini wasanii wetu wengi ni wasanii ambao wanapenda kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa. Wengi wao ni watu wa kupenda kusifiwa uongo Zaidi, chukizo kwao ni pale ambapo utamwambia jambo ambalo haliko sawa juu yake ambalo huenda likawa halina faida katika muziki wake.

Basi  hapo chukizo huja kwake kwa kujiona yupo sawa Zaidi lakini kuona yakuwa ambaye atasimama kwenye ukweli ni adui yake. Lakini katika uhalisia ni wazi akuambiae ukweli ni yule akutakiaye mema.

Andiko hili  Ni aibu Young Killer kuweka wimbo wake kwenye channel ya Harmonize. Limeasabisha Young Killer kuamua kuiblock kabisa Tizneez katika mtandao wa picha.

Jambo hili si jema kwa yeye kufanya hivyo, kwa maana inaonyesha namna ambavyo amechukulia ukweli kuwa chuki na sio kutaka kufahamu namna ambavyo ataweza faidika na muziki wake kupitia mtandao wa Youtube.

Lakini hatupaswi kushangaa haya maana waswahili husema “Mchunga peku hapendi ila hana viatu” (Akili)

Moja ya wasanii wakongwe na wenye heshima kwenye muziki wa kizazi kipya Afande Sele aliwahi kusema katika wimbo wake wa Mayowe “Naelewa hii ni fani na msanii sipo mwenyewe ili nifanikiwe inahitaji nikosolewe  na inapobidi nisifiwe”

Ni wazi yafaa kuishi kwenye hekima na busara za msanii Afande Sele kwa maana ukosoaji na kusifu kuwepo kwa lengo la kuendeleza msanii kuweza kufanikiwa Zaidi kupitia Sanaa yake.

Hivyo basi katika ukosoaji wa ukweli katika kujenga Zaidi muziki wetu wala haipaswi iwe chukizo kwa msanii/wasanii wetu kwa maana ya kuendelea kukua na kufaidika na muziki huu kwa sasa na baadae.

#TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa