“Enyi wajinga, fahamuni werevu, Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu” Dulla Plannet na Diamond Platnumz

“Enyi wajinga, fahamuni werevu, Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu” Dulla Plannet na Diamond Platnumz

Ama kweli! “Hakuna shule ya akili” bali ufahamu wa kila mmoja kwa upana wake. Upotoshaji ni mkubwa mno juu ya Dulla Plannet Mtangazaji wa Eatv/Ea Radio na Diamond Platnumz na team nzima ya Wasafi.

Ila ni kazi ngumu kuwaaminisha watu ukweli ambao tayari wao wana uongo wao kichwani. La! hasha hatuwezi kuchoka kuhubiri ukweli uliopo.

Ingawa yapasa “Usiseme masikioni mwa mpumbavu, maana atadharau hekima ya maneno yako” ila hapana kwa hili wacha tuseme ile kweli yenye kweli ili ituweke huru.

Kuzimwa kwa kusikika kwa Diamond na Team yake katika vituo hivyo ya Eatv/Ea Radio wala hapaswi kulaumiwa Dulla. Kwa maana ya uhalisia Dulla ni mwenye jina kubwa ila kiutendaji kwenye ofisi ni mtu mdogo mno, ambaye hupewa amri kama apewae mtu mwingine yoyote katika ofisi yoyote ile.

Ila swala hili limekuwa likichochewa zaidi na wachambuzi wasio na hoja waliojaa uteam na upendeleo wa upande mmoja ambao huandika bila kujua kile ambacho anaandika.

Ni wazi jamanI tusishangae haya kwa maana “Mchunga peku hapendi ila hana viatu” (Ufahamu).

Uhalisia ni kwamba ni kawaida mno kwa media kuzima kupiga nyimbo za msanii yoyote. Na hii huja pale msanii anapoenda kinyume na matakwa yao media husika.

Na hata kama mtangazaji mmoja ana tatizo na msanii fulani ni ngumu kwa nyimbo kuacha kuchezwa, isipokua katika kipindi chake tu. Ila vipindi vingine vitaendelea kucheza nyimbo za msanii huyo. Ila kama tatizo limehusisha uongozi ni lazima vipindi vyote vizime kupiga nyimbo za msanii husika.

Sasa tutafakari kwa upana je!kweli Dulla kwa nafasi yake ya utangazaji anaweza kuzima kupigwa kwa nyimbo za Diamond au msanii mwingine katika Eatv/Earadio?

Nguvu ya kuaminisha mashabiki wa Diamond kuwa Dulla ni chanzo cha kuzima kupigwa kwa nyimbo za Diamond na Wasafi kwa ujumla ni kubwa. Na imani ya kuamini inaendelea kupanda.

Ila msisahau hekima za maneno ya wahenga ya kwamba “Mjinga husadiki kila neno” Kimsingi haipasi hata kidogo kuendelea kumnenea Dulla lugha mbaya. Bali kutakari hoja zaidi na undani wa jambo.

Lakini kama mbwa aludiavyo matapiko yake, ndivyo mtu mjinga anavyorudia upambavu wake” (Mchambuzi)

Kwa maana ya wale ambao wamejivika uchambuzi wa kimuziki ila kiuhalisia hawana uwezo wa uchambuzi huo. Nyakati hizi sio njema kwa mchambuzi kuchukua upande mmoja kwa namna ya kutaka maslahi binasfi huku ukichafua maslahi ya mwingine.

Ni vyema kuchambua jambo ambalo unalifahamu kwa maana haya tuyaandikayo yanaishi lakini kusomwa kwa watu walio wengi.

“Iseme kweli yenye ukweli” kwa maana ya kusimama kwenye ukweli sio ushabiki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa