Dully Sykes Anafahamu yakuwa muziki umebadilika?

Dully Sykes Anafahamu yakuwa muziki umebadilika?

Huwezi kutaja wasanii bora 10 wa muda wote bila kutaja jina la Dully Sykes, ambaye ni wazi ni moja ya wasanii ambao wamechangia vyema kukua na kuenea kwa bongo fleva ndani ya nchi lakini pia nje ya nchi.

#TuzungumzeMuziki ni wazi wimbo wake mpya Bombadier ni wimbo ambao umeendelea kuonyesha yakuwa huu muziki wa bongo fleva ni wake kwa namna ya jinsi anavyoweza kwenda sawa na kasi ya damu changa ambayo inapenda Zaidi aina ya muziki huo.

Wimbo wa muziki umebadilika ni wimbo ambao unaimbwa na watu wengi kuanzia shabiki, media, wasanii na wadau wengine wa muziki.

Lakini katika uhalisia wasanii wengi na watu wengine wenye ushiriki wa muziki hawajui ukisema muziki umebadilika yapasa uende sawa na kasi husika ya mabadiliko hayo.

Tukisema muziki umebadilika tunagusa katika mambo yote yenye kugusa muziki katika utendaji na uendeshwaji kuanzia kwa msanii husika mpaka wadau.

Kitendo cha mkongwe Dully Sykes kulalama yakuwa wasanii hawajaposti kazi yake mpya kwenye mitandao ya kijamii ni wazi inaonyesha ni jinsi gani hafahamu ya kuwa muziki umebadilika. Dully ametoa malalamiko yake kwenye kipindi cha New Chapter katika kituo cha Radio Free Africa.

Lakini waswahili husema “Ni kheri kufa macho kuliko kufa moyo” Ni wazi Dully ni msanii ambaye anaonyesha namna ambavyo amekufa moyo kwa maana yakutaka Zaidi nguvu ya wasanii wengine wa sasa katika kumposti ila watu waone kazi yake Zaidi.

Lakini nyakati hizi si nyakati za kulalama yakuwa msanii hajaposti kazi ya msanii Fulani kwa maana yakuweza kutumia kurasa zako za mitandao ya kijamii na kuweza kufikia watu wengi Zaidi tena kwa kuchagua eneo ambalo unataka. (Promote)

Hivyo kwa mabadiliko ya muziki hasa kwenye mitandao ya kijamii ni wazi kaka yetu Dully alipaswa kutumia njia ya “Kupromote” kupitia kurasa zake na sio kutaka wasanii wamposti. Zama za nisaidie kushare ni wazi yapasa zipite isiwe ni lazima msanii aposti, bali aposti akijisikia lakini si kwa mlengo wa kutoa msaada.

Team Tizneez inawakaribisha wasanii wenye uhitaji wa kupromote kazi zao kwenye  mitandao ya kijamii email ni tizneez@gmail.com #TuzungumzeMuziki.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa