Dully Sykes ana tatizo la Young Killer kwa Harmonize

Dully Sykes ana tatizo la Young Killer kwa Harmonize?

Kudamshi ni wimbo mpya wa mkongwe Dully Sykes akiwa na Harmonize. Hakika wimbo huu una uzito wa juu katika usasa.

Ni wazi ghahabu ya Harmonize katika kuonyesha ukuaji wake wa uimbaji wa kila leo ni mfano wa simba dume mwenye manyonya mengi shingoni angurumapo nyikani.

Lakini ngurumo yake haikuweza fua dafu mbele ya mkongwe mwenye ladha tamu na ya ubabe kwenye muziki wa bongo fleva, ambapo mfano wake ni mithili ya jangiri asiye na huruma nyikani mbele ya mnyama yoyote yule.

Changanyo lao wote wawili katika kila mosi na ubabe wake umezaa umbili mara mbili wenye ladha tamu juu ya wimbo wa Kudamsh.

Lakini mdundo wa Bonga kutoka Beta Sound unakamilisha ukamili wa wimbo huu katika namna ya chagizo na mapigo ya ala yenye kuvutia katika usikivu na uchezaji katika nyakati mosi.

Lakini Je!Dully Sykes ana tatizo la Young Killer kwa Harmonize? Hili ni swali la wajuzi katika upana wa sanaa kwa sasa.

Ikumbukwe 5/6/2017 Young Killer alitoa wimbo wa Unanionaje aliomshirikisha Harmonize. Ambapo wimbo huu umeweka kwenye akaunti ya Youtube ya msanii Harmonize.

Na moja ya swali kuu ambalo tulimuliza Young Killer ni “Kwanini wimbo wake ameweka kwenye akaunti ya Youtube ya Harmonize?.

Na majibu yake yalikuwa “Unajua tangu nianze muziki sijawahi kupata fedha kupitia Youtube, hivyo nimeweka kwa Harmonize ili niweze kupata fedha”.

Jambo hili kwetu halikuwa jema maana ni wazi tulitafakari katika upana wa maisha yote ya nyimbo na usawia wa mapato ya kila leo katika tazamo la mtandao.

Na tulijitolea katika kumsaidia Young Killer juu ya swala zima la yeye kuweza kupata fedha kupitia mtandao huo, lakini Young Killer hakuwa na shauku ya msaada huo kesho zikawa nyingi mpaka leo hii. (Fedheha)

Na leo tunaona tena mkongwe Dully Sykes ameweka wimbo wake katika akaunti ya Harmonize je! na yeye ana tatizo kama la Young Killer kiasi cha kuweka wimbo huo?.

Ikumbukwe uwekapo wimbo katika mtandao huo hakika mfumo wa malipo utaendelea kwa mhusika mwenye akaunti yake sisi mwingine.

Je! makubaliano yakoje? kuanzia nyakati hizi za maelewano mpaka nyakati zijazo ambazo huenda kukakosekana maelewano je! uhalisi utakuaje?.

Katika swala zima la hatimiliki ya wimbo ni vyema msanii kusimamia simamio la umiliki hasa maana muziki ni bidhaa ambayo huuza nyakati zote.

Umakini unahitaji kwa mapana yake katika kesho ya msanii kwa upana wa familia yake.

Hivyo bado hatujajua hasa kipi kimefanya Dully Sykes kuweka wimbo huo kwenye akaunti ya Harmonize?.

Ni changamoto kama za Young Killer au? nini ambacho kipo?

Itaendelea….

#TuzungumzeMuziki