Dudu Baya ni mfa maji haki yake kutapatapa.

Dudu Baya ni mfa maji haki yake kutapatapa.

Tujifunze tafakari ya mengi kabla hatujachachawa na machache yasiyo na maana. (Upuuzi)

Sisi hatujawahi kuyumbishwa wala kuweka zingatio la lolote kutoka kwa Dudu Baya, achilia mbali nyakati za uzamini kwenye muziki  wake. (Kweli)

Nyakati hizi tuweke zingatio kwa lipi? Matendo yenye kiki? au uropokaji wa hovyo uliojaa soni? (Ajabu).

Na hatuweki zingatio kwa maana upuuzi umejaa katika uhalisi wake. Kuzungumza utamduni wa hiphop na dhihaka ya wengi ambao wapo katika tamaduni kubadilika hakika ni hovyo yenye hovyo. (Uhalisia)

Lakini hatushangazwi nae kiasi cha watu wanavyoshangaa kwa maana hata mswahili hunena “Uzuri wa godoro wa nje tu, ndani mna pamba” (Ufahamu)

Ikumbukwe Dudu Baya ambaye anasema leo hii watu wa hiphop wabadilike ndiye yule yule ambaye kwa miaka kadhaa nyuma alikuwa muumini wa utamaduni huu. (Ndiyo)

Sasa nguvu ya kunena watu wabadilike inatoka wapi? Ni wazi ni katika kiki yenye hovyo ili watu wenye utamaduni wao wampe majibu mengi. (Uhalisia)

Ni wazi uisho wake wa sasa ni katika kusema semi nyingi zenye hovyo ili tu aweze kupata majibu ya wengi na aendelee kuwepo midomoni mwa watu. (Hakika)

Tunapenda kila msanii afanye kwa sanaa yake ambayo yuko na uwezo nayo, kama Dudu Baya hiphop ilimshinda ni vyema akae kando si kuleta semi nyingi za hovyo. (Naam)

Okoa Hiphop ni jambo lenye kuheshimiwa zaidi ambalo hakika mafanikio ya jambo hilo lilikuwa ni kwa ukubwa. (Naam)

Adili Chapakazi ni muanzilishi wa jambo la Okoa Hiphop ambapo ni mwaka 2006 ndiyo ilikuwa uzao wake. (Hakika)

Na mitaa ikaelimika vyema kupitia Okoa Hiphop, vivyo basi ni vyema Dudu Baya akawa kimya katika kusema vibaya utamaduni wa hiphop na harakati za Okoa Hiphop. (Uhalisia)

Lakini ndugu zetu wa utamaduni wa hiphop ni vyema mjue yakuwa “Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano, Upumbavu wake hautamtoka” (Ndiyo)

Leo hii tunapaswa tujiulize swali,Dudu Baya anafanya muziki wa aina ipi?. Ni msanii mwenye upana wa kipawa cha uhakika? Sasa unadhani atafanya nini zaidi ya afanyacho? (Chekesho)

Lakini ndugu zetu si mnajua kuwa “Kipimo cha akili si ukubwa wa mwili wala umri bali akili yenyewe” (Eeh)

La! hasha ni vyema mjue “Hakuna muziki usiokuwa biashara” Simamio sanaa uwezavyo ifanye kwa upana wa kuongeza wateja kila leo. (Muziki)

#MuzikiNiSisi