Dubo Hawa marapa wenu kumbe bora hata ya Shetta

Shettakororobo

DUBO: HAWA MARAPA WENU KUMBE BORA HATA SHETA

_______

Kuna wachanaji wengi tu katika nchi hii hata nje ya nchi ambao walikuwa na ndoto na bado wana ndoto ya kufanya kazi na Duke. Duke ni mmoja kati ya maprodyuza ambaye ukimuondoa majani ndiye atakayekuwa ame-inspire maprodyuza wengi waliopo sasa katika ulimwengu wa Hip Hop Tanzania. Sio rahisi zikapigwa nyimbo kumi za bongo Hip Hop alafu usisikie ngoma ya duke au prodyuza ambaye anaiga upigaji midundo wa duke.

Ni kweli wasanii wengi hawajafanya kazi na Duke. Kitu ambacho wasichokijua watu wengi ni kwamba hata wachanaji wengi walioko katika Familia ya Tamaduni muzik ambayo anatoka Duke hawajawahi kufanya kazi naye na wengine bado wana ndoto hiyo. Huwezi kuamini hata Nash Mc ukiondoa kushirikishwa kwenye kibao cha “Kilinge” kwenye kanda mseto ya “Underground Legendary” hana kazi nyingine aliyofanya na Duke ambayo amekwishaachia.

Pointi yangu ni kwamba kufanya au kutokufanya kazi na Duke hakukufanyi kuwa mchanaji mzuri mfano ni Suma Mnazaleti ambaye alishiriki katika kibao cha “Hisia” na hakuwa na uwezo wa kupanga vina. Mwisho wa siku akaishia kuimba kwaito na kiduku na ndiye anayeendelea kueneza dhana kwamba Hip Hop zinazofanywa na watu kama Duke ni ngumu na hazilipi.

Nakubaliana kabisa na Dubo anaposema kwamba Msimshushe bei kisa hamjamsikia kwenye mixtape ya Duke au Ray Teknohama. Kufanya kazi na maproduza hao sio guarantee ya kuwa mchanaji mkali. Sikushangaa siku nilipokutana nae karibu na studio ya Mensen akaanza kutoa maneno ya shombo kwamba “washkaji wa Kilingeni njaa kali”. Ndio maana dubo anakemea kwamba “ni usnitch kuacha misingi kifala na kuamini Hip Hop sio muziki wa Biashara”.

Katika mazungumzo binafsi niliyowahi kufanya na Duke aliwahi kusema kuhusu Hip Hop kutokuwa muziki wa Biashara na kampeni ya kuipiga vita ni dhana potofu. Alitoa mfano wa soko ambalo huwa na bidhaa nyinginyingi hivyo msimu wa bidhaa moja hauwezi kuathiri uwepo wa bidhaa nyingine. Kinachofanyika sasa ni kulazimisha Hip Hop isiwepo kisa ni msimu wa Bongo Fleva.

Dubo anaamini kwenye underground Hip Hop ambako kina duke na maprodyuza wengine wanaishi ndiko anakoweza kufanya kile anachotaka tofauti na wachanaji wa mainstream ambao hutakiwa kubadilika badilika kulingana na vyombo vya habari vinavyotaka.

Nadhani Dubo anapata utata na mifano halisia ya watu wake wa karibu ambao wametwist kidogo kutoka katika midundo ya Handakini na kutumia ile inayopendwa na watu wa Mainstream je wamepata mafanikio gani. Dubo akajikuta anasema hawezi kukasirika mtu mwingine anapofanya Trap ili apate dau ila akawaonya kuwa kama wanaamua kuacha misingi kwa sababu ya shilingi wahahakikishe wanazipata maana kuna wengine wameacha misingi ila shilingi hawajadaka.

Nilishituka kidogo kumsikia Dubo akisema yeye ni nikki mbishi wa pili, Dubo ni Langa ni Langa ni Fid Q ni Joseph Haule. Nikawa najiuliza Dubo anataka kuwa Nikki Mbishi wa “Jogoo” au wa “Indebe”, Anataka kuwa Fid Q wa “Profesheno” au wa “Walk It Off” au labda Dubo anataka kuwa Profesa Jay wa “Chemsha Bongo” au wa “Kamili Gado”. Nikabaki njia panda.

Hawa wanahiphop wa leo wamekumbwa na nini? Mbona zamani mlituambia Hip Hop iko hivi leo mbona mnatuambia iko vile. Naanza kumkumbuka yule Kala Pina aliyekuwa na vita kubwa na Bongo Fleva/Wabana pua kwa miaka mingi. Miaka ya hivi karibuni amejikuta akifanya kolabo na Q Chilla na Ommy. Naanza kumuelewa mchanaji anaposema “Kuwa Hip Hop sio kumchukia Jux na Dangote”

Ndio!! Namuelewa Dubo anaposema hivyo. Kama huna uhakika kama utabaki Underground milele ni vema kuweka akiba ya maneno. Siku underground Hip Hop ikikushinda itabidi uwarudie wabongo fleva upige nao collabo. Sasa kuna haja gani ya kuwapaka shombo wakati huna imani na unachokifanya. Jihadhari usije kulamba matapishi.

Pia nakubaliana tena na mchanaji anaposema “kuwa hip hop sio kumchukia Jux na Dangote” kwa maana nyingine mchanaji katumia Lugha ya picha kumaanisha kuwa Hip Hop sio kuikosoa Bongo fleva tu kuna mambo mengi sana ya kuchana. Kila mc siku hizi anataka kuichana Bongo Fleva tu utadhani mada zingine hakuna. Kuna changamoto nyingi za kijamii ambazo hazijatupiwa macho ila maemc wa bongo wameegemea kuwachana waimbaji wa Bongo Fleva ambao hawana hata muda wa kuwajibu. Hii inawafanya hata wachanaji chipukizi kukua wakiamini kuichana Bongo Fleva ndio Hip Hop.

Mapacha enzi za vinega na mixtape ya antivirus waliwachana sana wabana pua hususani diamond na wasanii wa THT achilia mbali Ruge ambaye ni kama dhima ya mradi mzima ilikuwa ikimlenga yeye. Baada ya miaka kadhaa kupita wakaomba kuyamaliza na Ruge. Dubo anawakumbusha kwamba msijidanganywe na wadau kwamba mmeyamaliza kwasababu mlishawachana sana mpaka kwa matusi na msidhani kwamba wamesahau.

Kilichofanyika kilikuwa na kutaka jamii ione kwamba hamkuwa sahihi kwa harakati mlizokuwa nazo ndio maana waliulizwa maswali ya kimitego mitego kwenye XXL nao wakaingia mtegoni. Hata sikushangaa baada kutoa wimbo wa “Time For Money” ukapigwa kidogo ukawekwa kapuni na sikumbuki kama walishapewa show na clouds zaidi ya Fiesta ya Moshi, 2014.

Nihitimishe kwa kukubaliana na Dubo pale anaposema kwamba “Hawa marapa wenu kumbe bora hata shetta”. Maana shetta tangu anaanza muziki alijulikana yeye anasimamia nini. Marapa wetu wa leo anatuaminisha hivi kesho anatuaminisha vile. Kuweni makini na kauli zenu. Huu ni mtazamo wangu masela msijenge chuki.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na

Malle Hanzi
O715076444
©2016