Dr Mengi anahusikaje kwenye muziki wa kizazi kipya? (Ulizo

Dr Mengi anahusikaje kwenye muziki wa kizazi kipya? (Ulizo)

Historia hazina nafasi kubwa katika maisha ya kizazi cha mtandao, bali matendo yenye ukamili katika nyakati. (Uelewa)

Lakini muziki huu wa kizazi kipya shukrani kuu zapasa ziwepo kwa Mzee Mengi, tena kwa hali ya ukubwa. (Kabisa)

Historia ya muziki huu ni ndefu mno tangu 1989 mpaka sasa 2019. Lakini daima historia haijawahi kufutika kwa wajuzi. (Hakika)

Radio One katika kipindi chake cha Dj Show ndiyo kipindi cha kwanza kupiga muziki wa Bongo Fleva radioni. (1996)

Na tangu hapo upana wa muziki wa kizazi kipya ni leo tunatazama ni kwa namna ipi umeokoa maisha ya familia nyingi zaidi. (Ajira)

Kabla hatujasema hongera kwa mpwa wetu Mike Mhagama (Mtangazaji) ni vyema tutangulize heshima kwa Mzee Mengi kwa kuwa ni mtu wa kwanza kumiliki kituo binafsi na chenye Fm maana enzi hizo ilikuwa ni Am. (Pongezi)

Lakini hatuwezi kusahau kumbukumbu za kaka yetu Taji Liundi ambapo ni wazi hakuna asili ya bongo fleva bila yeye pia. (Mchango)

Maana historia inatuonyesha yakuwa Taji alikuwa ni muasisi na muanzilishi vilevile mtayarishaji wa kipindi cha Dj Show. (1994)

Lakini kwa Mzee mengi licha ya umri wake na heshima yake hakusita kutoa nafasi au kuwa mchoyo kwa vijana juu ya kile waamicho. (Muziki)

Ni wazi mchango wa kuanza kupiga nyimbo za bongo fleva radioni si jambo dogo ikumbukwe enzi hizo muziki huu ulikuwa ni onekano la uhuni zaidi. (Muda)

Hivyo “katikati pasiwachanganye mkasahau chanzo” Mzee mengi ameigusa mno Bongo Fleva kwa namna hii. (Uhalisi)

Na leo amepumzishwa kwenye makazi yake ya milele huko Mkoani Kilimanjaro kwa sisi waswahili tunaamini yakuwa “Hata kufa ni kuishi ilihali ni kuishi katika kifo” (Sikitiko)

Hatuna la ziada zaidi ya kunena umemaliza mwendo wa duniani mzee Mengi, maisha ya kupumzika katika kifo uwe nayo mema. (Pumzika)

#MuzikiNiSisi