Dogo Janja huenda akapitia aliyopitia Ben Paul na Ommy Dimpoz.

Dogo Janja huenda akapiitia aliyopitia Ben Paul na Ommy Dimpoz.

Kumekuwepo na maneno mengi juu ya Dogo Janja ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya na Irene Uwoya ambaye ni muigizaji toka uwanja wa bongo muvi. Maneno haya yamekuwepo Zaidi kwenye mtandao wa picha Instagram yakuwa wawili hawa wamefunga ndoa.

Lakini wengine wakisema ni kiki tu ya wimbo mpya wa Dogo Janja.

Maoni ya wasomaji wetu ni mengi yakuwa Tizneez mbona hatulisemei kitu jambo hili? Ni kweli sisi huwa kimya kwenye mambo haya ambayo tunakuwa hatuna undani nao lakini sisi wakati wote huzungumza muziki si kitu kingine.

Ila kwa kuwa wengi mmeonyesha kuwa mnataka tusema jambo, tumeona wacha tuseme.

Sisi tunatazama Zaidi kwenye muziki wa Dogo Janja kama ni kweli amafunga ndoa ni jambo la kheri mno kwa maana ndivyo utaratibu wa maisha unavyotaka.

Lakini kama amefanya kiki ni wazi atakuwa amejichimbia shimo na kuungia wakati huo kiki yake kumfunika vyema.

Kuna mifano mawili katika haya maswala ya kiki. Moja ikiwa ni wa Ommy Dimpoz katika wimbo wa Wanjera ambapo kabla ya kutoka kwa wimbo huo aliposti picha akiwa na Wema Sepetu kama mpenzi wake ilihali alimtumia kama video queen tu.

Hivyo kiki hii ilizidi wimbo husika na wimbo ukashindwa kufanye vyema maana watu walikuwa wakizungumza kuhusu ukweli uko wapi kati yake na Wema Sepetu.

Lakini mfano wa pili ni Ben Paul mara baada ya kupiga picha zake ambazo zilionyesha uwazi mkubwa wa mwili wake hasa maeneo ya nyuma na baada ya muda mfupi kuachia wimbo ni wazi watu walibaki pale kwenye picha tu na sio wimbo tena.

Hivyo wimbo wake ukapita bila mafanikio yoyote kwa maana kiki ilizidi wimbo husika.

Hivyo jambo hili huenda likajirudia tena kwa Dogo Janja kama tu atakuwa ametumia kiki ya kufunga ndoa na Irene Uwoya.

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa