DIAMOND PLATNUMZ NI KWELI AMESAHAU KAULI YAKE?

p031h93x

DIAMOND PLATNUMZ NI KWELI AMESAHAU KAULI YAKE?

“Usitukane mamba kabla hujavuka mto” moja kati ya misemo iliyomingi ambayo mara zote hupenda kuitumia katika shughuli za kila kila siku hasa katika kazi yangu pendwa ya uandishi.

Wapo wachache wenye kusema mkamilifu ni mtu ambaye ameshatoweka katika uso wa dunia, sasa naanza kuamini katika hilo. Maana wengi husema mengi wakati wapo katika nyakati fulani, ila imani yangu inaniambia tena kuwa wengi hawawezi kusimama katika maneno ambayo huyasema katika nyimbo, maandiko na hata katika mahojiano.

Muziki gani ni wimbo ulikuwa na hati miliki ya msanii Nay wa Mitego ambapo alimshirkisha msanii Diamond Platnumz, katika kumbukumbu zangu wimbo huu ulitoka miaka miwili nyuma tangu sasa 2016. Hakika wimbo huu ulifanya vyema hata kuweza kushinda tuzo ya kadhaa katika tuzo za KTMA.

Wimbo huu wa Muziki gani ulikuwa katika aina ya majibizano kati msanii wa bongo fleva na msanii wa hiphop, katika mistari iliyoko humo kuna mengi yalizungumzwa ambapo katika uhalisia ni wazi yaligusa ukweli katika kiwango cha juu. Ikumbukwe wimbo huu uliweza kuwa vichwani mwa watu ndani ya saa chache tangu kutoka kwake, licha ya kuwa ni wimbo uliopata kupakuliwa kwa muda mfupi na watu wengi katika blog mbalimbali.

Hakuna jambo jema kama kusimamia msimamo wako, hasa katika nyakati hizi ambapo walio wengi hutunza kumbukumbu kila iitwapo leo. Wengi hujivuruga wenyewe katika mambo mengi yasiyo na msingi ila kwa nyakati unafanya huona lina msingi.

Ni kheri kujikwaa kidole kuliko ulimi” Msemo huu unanirudisha miaka miwili nyuma pale ambapo msanii Diamond Platnumz aliimba mistari inayosema “mimi nina mengi ninayajua ila wewe mtemi utaanzisha utata michezo yenu kutoboa pua bora ninyamaze utanipiga mbata.”

Katika mistari hiyo ni wazi ilikuwa ni shambulio kwa msanii wa hiphop Chid Benz ambaye kwa wakati huo alikuwa ametoba pua na kuweka kipini katika pua yake, jambo ambalo lilishangaza walio wengi. Hakika Chid Benz alikuwa msanii wa kwanza wa muziki wa kizazi kipya kutoboa pua.Mistari hiyo ilivunja urafiki ambao ulijejengeka kati ya Diamond na Chid Benz, ambapo urafiki huo ulirudi mwaka 2015 pale Chid Benz alipofanya wimbo na Diamond pamoja na Dully Sykes.

Ni siku ya 7 sasa tangu msanii Diamond Platnumz kuweka picha katika mtandao wa picha Instagram ikionyesha akiwa na kipini katika pua yake, ambapo ni wazi ametoboa pua. Maoni kutoka kwa watu yalikuwa mengi, licha ya maoni lugha kali ilitawala katika picha hiyo na wengi wakiwa wamesahau ule msemo usemao “Kipendacho roho ni dawa”. Sidhani wala sifikirii kama Diamond alitoboa pua kwa kulazimishwa, isipokuwa mapenzi yake toka kwenye uvungu wa moyo wake.

Si mwepesi sana katika kujaji kile mtu anachokiona sawa kwa upande wake, pia ukumbuke ule usemi wa msanii wa hiphop Fid q ambapo aliwahi kusema “Ustar hauji bila skendo” inanipa wakati mzuri kulinganisha matukio katika kutoboa pua na lile la kuanzisha kipindi cha Runinga kitakachokuwa kinaonyesha maisha yake ya kila siku Diamond Platnumz.

Licha ya kutafakari kweli amesahu kauli/alichoimba miaka miwili nyuma kuhusu kutoboa pua?.Wapo mashabiki wake ambao wanaona kama Diamond amefanya kosa kutoboa pua na hata kusema hawataweza tena kumshabikia. Mwanzo niliona ni hoja dhaifu eti kuacha kumshabikia Diamond kisa ameamua kutoboa pua. Ila nyakati zinaenda huku nikitafakari kwa kina na kugundua mambo kadhaa.

Unaweza kujiuliza kwani kutoboa pua na muziki wake vina uhusiano gani?mpaka walio wengi kusema hawataki tena kumshabikia?. Katika uhalisia watu hupenda kushabikia msanii katika mambo yote kuanzia muziki wake mpaka hata undani wa maisha yake. Kitendo cha Diamond kutoboa kuna mambo ambayo yanatokea sasa kwa upande wa soko lake muziki hapa Tanzania.

Bado watanzania tunaishi katika mila na desturi ingawa wachache wameonekena kuzikataa lakini nguvu ya kupinga mila na desturi ni ndogo, kuliko nguvu inayozikubali. Kitendo cha kutoboa pua Diamond ni wazi kimempotezea mashabiki hapa nyumbani, ila inaweza kuwa kimemuongezea mashabiki wengi katika soko la kimataifa. Ila msiache kukumbuka” Mcheza kwao hutunzwa”.

Sio mbinafsi katika kusikiliza mitazamo ya wapenda muziki wa bongo fleva, maana pia huniongezea kujua yaliyomengi hususani katika muziki huu wa bongo fleva unaondelea kukua siku baada ya siku. Wapo pia wanaosema kuwa anguko la Diamond katika muziki limefika, huku wakifananisha kile kilichotokea kwa Chid Benz baada ya tu ya kutoboa pua haikuwa rahisi tena mashabiki wake kupokea kazi zake kama ilivyokuwa mwanzo.

Bado tuna muda mzuri, huwa sipendi pia kutumia hisia zaidi katika uchambuzi wa muziki huu. Ila ikumbukwe “Hakuna marefu yasiyo na ncha”

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez