Diamond Platnumz hajatumia ufahamu, bali kuendeshwa na hisia zenye hisia.

Diamond Platnumz hajatumia ufahamu, bali kuendeshwa na hisia zenye hisia.

Hisia zimemuedesha yakuwa akiweka mtandaoni video zake za faragha na wapenzi wake wawili atazungumzwa kwa ukubwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vipindi vya radio na runinga.

Ni wazi amezungumziwa kwa upana, ilihali ni katika kundi lipi? Ni kundi la udaku ambalo kimsingi haliwezi kumuongezea heshima bali kuipunguza kwa ukasi.

Lakini kama angetumia ufahamu wala asingeachia video hizo, maana katika kundi la wajuzi na wenye ufahamu ni dharau juu yake na kuona kuwa ni mwenye ufahamu mdogo yeye, wapenzi wake na genge lake kwa ujumla.

Sikitiko letu sisi Tizneez ni mtu kama yeye kuwekeza kwenye kiki za kipuuzi Zaidi. Lakini tukirejea semi ya mswahili yakuwa “Usigombane na mkwezi nazi imeliwa na mwezi” (Ufahamu).

Hakika inatupa Amani ya kusema mengi yenye kujenga juu yake lakini wasanii wengine.

Ni wazi miguu yake ilipaswa kuzikimbia kiki za kipuuzi bali kufuata kiki zenye maana, ambazo zitazidi kumpa heshima ya kila leo.

Leo kila mmoja anafahamu mafuriko yaliyoko Jiji Dar es Salaam hakika ni tangu jana na leo mitaa mingi imekuwa mibaya kupita kiasi.

Na moja ya maeneo ambayo pia yana changamoto ya mafuriko ni pamoja na mtaa wake aliotokea wa Tandale.

Tuligemea kuwaza katika upana wa kutoa pole kwa wakazi wa Tandale lakini hata pole ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam lakini hata kwa ngazi ya Tanzania nzima.

Lakini kufika baadhi ya maeneo na kuweza kushikana na wananchi katika mengi juu ya mafuriko hakika jambo hili lingemsogeza mbele Zaidi.

Maana Diamond ni kioo cha jamii hivyo jambo hilo lingefariji kwa upana. Lakini hisia zenye hisia zimemfanya ajivue nguo hadharani huku akidhani yakuwa ni mafanikio. (Fedheha)

Lakini nyakati zote “Utu busara ujinga hasara”  la!hasha tusisahau yakuwa “Mtembea peku hapendi ila hana viatu” (Ufahamu)

 

Ni wazi kama angeshikamana na wakazi kadhaa wa Jiji la Dar es Salaam hakika ingekuwa ni kiki njema na nzuri, huku akiandamana na genge lake la wcb hakika ingekuwa faraja na kujizolea sifa zenye faida.

Ni vyema wasanii mfikiri katika kiki zenye maana, kiki za kuvua nguo hadharani na video za faragha haziwezi kuwapa heshima bali fedheha ya wakati wote.

Naam! Na mwenye hekima asikiye na kujiongezea ufahamu katika andiko hili, bali mpumbavu kushikama na upumbavu wake katika kuharibu kesho yake. Tafakari.

#TuzungumzeMuziki