Diamond Platnumz chanzo kikuu cha kumfukia Fid Q shimoni.

Diamond Platnumz chanzo kikuu cha kumfukia Fid Q shimoni.

“Urafiki sio urafiki usipochanganywa na kazi” hii ni moja ya sentensi kutoka kwa Fid Q ambaye ni miongoni mwa watu wetu wa karibu sisi kama Tizneez.

Lakini licha ya ukaribu wetu hatuzuii kusema ile yenye kweli  ambayo daima tumekuwa tukiihubiri kila iitwapo leo hapa Tizneez.

Mashabiki wengi walikuwa na kiu na muziki wa Fid Q ambaye katika uhalisia huwezi kuzungumzia Bongo Hiphop bila kumtaja Fid Q. Na hakika mwezi mmoja kama sio wiki kadhaa nyuma aliweza kukata kiu yao baada ya kuachia ngoma mbili katika wakati mmoja.

Ulimi Mbili na Fresh ni mbili zilizoachiwa kwa wakati mmoja ambapo katika uwazi mapokeo ya Fresh yalikuwa makubwa katika vijiwe vingi vya hiphop.

Na hakukuwa na wakupinga juu ya uzuri na ukubwa wa wimbo wa Fresh kwa maana “Wengi wape”.

Lakini katika muda mchache kulitoka Remix ya wimbo wa Fresh ambayo kiupana hatudhani kama ilikuwa katika mipango yake ya kutoa remix hiyo katika muda mfupi kiasi hicho.

Fresh Remix alisimama Diamond Platnumz, RayVany na mmliki halali ambaye ni Fid Q.

Katika upana Fresh Remix ilikuwa ni bora pia lakini wimbo hakuweza kuzungumziwa bali kuzungumziwa kwa vipande vya Diamond ambavyo vilionekana kumgusa mpinzani wake Ali Kiba.

Lakini katika shimo zuri la kuua Fresh Remix tena ni pale ambapo Diamond alirekodi verse ya sekunde 34 ambapo alitumia tena mdundo huo kusema mengine kuhusu Ali Kiba na Ommy Dimpoz.

Ni wazi kilichofuata hapo ni maneno mengi katika mitandao ya kijamii ambayo ni wazi hayakuwa yanamuhusisha Fid Q wala wimbo wake wa Fresh bali Diamond na Ali Kiba.

Hivyo ni wazi upepo uliovuma kati ya Diamond na Ali Kiba umeweza kuipoteza Fresh kiwepesi mno.

Ila Fresh imeendelea kubaki kwa wale ambao ni mashabiki halisi wa Fid Q na katika ile kweli yapasa kila wimbo uweze kuongeza mashabiki wapya katika msanii kukuza na kueneza Sanaa yake. lakini “Daima subira yavuta kheri”

Hili halina kipingamizi yakuwa Diamond ndiyo chanzo kikuu cha kumfukia Fid Q shimoni na wimbo wake wa Fresh.

Hivyo katika upana bado Fid Q anabaki na deni la wimbo kwa mashabiki wengi Zaidi ukitoa wale ambao yupo nao sasa.

Hakika “Wapiganapo fahali wawili ziumiazo ni nyasi”

#TuzungumzeMuziki

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa