DHARAU HUANGUSHA WENGI WENYE VIPAJI “ HANSCANA”

11820714_649999765102448_1875389659_n

“DHARAU HUANGUSHA WENGI WENYE VIPAJI “ HANSCANA”

Hakuna jambo jema kama kukumbushana yaliyo mema katika maisha ya kila siku, moja kati ya mengi yaliyo mema ni Nidhamu.

Nidhamu!!Nidhamu!!Nidhamu!neno dogo ambalo lina herufi saba tu, lakini katika hizo herufi saba kama utashindwa kuzitumia vyema utajikuta ukipoteza mambo mengi katika maisha yako. Ukikosa nidhamu si rahisi pia kuwa na rafiki katika maeneo yote kuanzia kazini, nyumbani, shuleni na sehemu nyinginezo ambazo zitakukutanisha na watu tofauti tofauti.

Watu wengi wamepoteza vitu vingi vya maana sababu ni kukosa nidhamu, watu wengi hawajui kama ukiwa na nidhamu lazima ufanikiwe katika kile ukifanyacho. Watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na nidhamu ya hali ya juu hutafakari kabla hajaongea/hajasema kuwa atakachosema kina umuhimu?kitampa heshima? Na je kitamsaidia nini?

mwenye hekima huona haya na kujificha, bali mpumavu huenda mbele na kuvimba kichwa” Mh Joseph Haule (Prof Jay)i. Hii ni moja kati ya kauli ambayo ndani yake imebeba ujumbe wenye kuonyesha mtu mwenye Hekima/Nidhamu anakuwa ni wa namna gani na asiye na nidhamu anakuwa ni wa namna gani.

Inachukua miaka mingi kujenga heshima, lakini kuishusha heshima yako ni kitendo cha sekunde moja tu kama sio nusu sekunde.

Namtazama kijana mdogo Hanscana kwa mapana zaidi, namfikiria katika maono mengine hakika ana kipaji kikubwa katika upande wa kuongoza video. Lakini ikumbukwe kipaji kinaongozwa na Nidhamu je unadhani ana nidhamu ya kulinda kipaji chake? Wapo wengi walioibuka katika Soka,Muziki, Utangazaji na sehemu nyingine lakini neno la herufi saba tu NIDHAMU limefanya wapotee katika anga zao ambazo walikuwa wakifanya vyema.

“Q Chillah amepitwa na wakati” Hanscana. Moja ya kauli aliyoitoa siku kadhaa zilizopita juu ya msanii Q Chillah.

Nidhamu ipo wapi kwa wasanii waliochonga barabara ya muziki huu Bongo Fleva/Hip hop? Si mara ya kwanza kusikia vijana walioibuka hivi karibuni kuongea kauli zenye kuonyesha dharau kwa wasanii wakongwe. Lakini moja ya vitu ambavyo wanasahau vijana wa sasa ni kuwa hawa wasanii ambao wamekuwa wakiwabeza kwa kejeli ndio wasanii waliofikisha huu muziki hapa ulipo.

Nidhamu iko wapi kwa muongozaji mchanga wa video Hanscana? Pengine yapo mengi yanayokudanganya kuwa sasa upo juu, inawezekana ingawa sina hakika kama upo juu, ila ambacho unatakiwa kufikiria je huko juu utakuwa kila siku? Nyakati hupita.Lakini kama hautatengeneza heshima/nidhamu kwa kile unachofanya haitakuja kuwashangaza walio wengi kutokuja kutambua mchango wako.

Nidhamu ni kitu pekee ambacho hata iweje yani hata kama utashuka kisanaa,kiuchumu, soka na mengineyio basi utaendelea kuishi katika kuheshimiwa, na hii yote inatokana na nidhamu. Ni vyema kuchunga ulimi wako katika mahojiano ambayo mara nyingi umekuwa ukiyapata sasa karibu kila siku.

Nidhamu iweke mbele katika kile ukifanyocho kila iitwapo leo, si kwa Hanscana tu ila kwa kila mmoja na katika sehemu yake. Kumbuka nidhamu haichagui mkubwa wala mdogo, mweupe na mweusi nidhamu ni kwa wote.

www.tizneez.com

Twitter tizneez

Facebook tizneez

Instagram tizneez

Youtube tizneez