“Dhana ya muziki biashara na mapokeo tofauti kwa wasanii”

“Dhana ya muziki biashara na mapokeo tofauti kwa wasanii”

Neno muziki biashara limekuwa ni neno linalosikika mno kutoka kwenye vinywa vya wengi hasa wasanii na watu wa media.

Usikikaji wa neno hili umekuwa ukichangia kuyumbisha wasanii hasa kwenye upande wa nidhamu kwa maana ya kufanya mengi ambayo yapo nje ya Sanaa. Wengi wamekuwa wakisahau licha ya kipaji lakini nidhamu itakufanya ufike mbali Zaidi kwa maana ya kujenga misingi iliyoimara.

Lakini mapokeo ya muziki biashara kwa wasanii wengi ni kufanya mambo ya hovyo Zaidi ili tu azungumziwe wakati huo akisahau nje ya Sanaa yake kampuni huenda ikamuhitaji ili kuweza kuwa balozi, lakini ni ngumu kampuni kumtumia msanii ambaye hana nidhamu ya kipaji chake.

Muziki biashara sio kuuza tu kwenye mtandao au kuuza kwenye matamasha ila kuuza hata maisha yako ya Sanaa kwa kampuni Fulani. Na hakika kwenye makampuni ndiyo kuna pesa nzuri, hivyo ni vyema kutumia muziki kama ngazi njema ya kupata mafanikio makubwa.

Muziki ni bashara kubwa mno, lakini bila umakini na mapokeo tofauti wa neno muziki biashara ni wazi tutaendelea kuwaona wasanii wachache wakiwa na mafanikio makubwa na wengi wakiwa masikini wenye majina makubwa.

Mwenye sikio na asikie lakini mwenye macho na aone mwenye kusoma na aelewe hakika bila nidhamu huwezi kufikia mafanikio. Muziki biashara tengeneza jina kuwa uzuri kwenye Sanaa yako uweze kutumika vyema na makampuni.

#TuzungumzeMuziki.