Dawa ya Chid Benz hanayo yoyote yule bali yeye mwenyewe

Dawa ya Chid Benz hanayo yoyote yule bali yeye mwenyewe.

Laiti kama Chid Benz angeishi katika maneno yake anayonena katika wimbo wa ‘Nipokee’ akiwa na Ben Paul hakika angekuwa mpya.

Lakini anaishi nje ya uhalisi wa wimbo wake wa ‘Nipokee’ ambao ni tungo zenye uhalisia wa maisha yake na wengine wengi.

Lakini ni nani awezaye kuweka maji kwenye kiganja na yasimwagike? hakika hayupo na hata kaa atokee.

Basi ndivyo ambayo haiwezekani kwa yoyote yule kumtoa katika shimo baya la matumizi ya dawa za kulevya Chid Benz.

Dawa yake hanayo mtu yoyote yule bali yeye mwenyewe, yapasa moyo wake uamue na utafakari namna ya dawa za kulevya jinsi ambavyo zinamfanya kuishi maisha mabaya zaidi.

Lakini sisi nyakati tunajawa na shangazo juu ya matumizi hayo nae yeye anatushangaa kwa kuona hatujui raha apatayo, ilahali kwa sisi ni janga kubwa.

Hata tupaze sauti kwa namna ipi hakika haiwezi kuwa msaada kwake, maana masikio yake hayana usikivu wa kusikia pema bali pabaya kwa upana. (Fedheha)

Yapasa moyo wake uamue yakuwa sasa naacha matumizi ya dawa za kulevya, hakika hii ndiyo dawa yake.

Lakini tusisahau semi ya mswahili yakuwa “Mkataa pema, pabaya panamuita” hakika ni uhalisi wenye uhalisia.

#TuzungumzeMuziki