Darassa ni kutwa mara tatu.

Darassa ni kutwa mara tatu. 

Leo ni wimbo wake ambao umeanzisha Jumatatu yetu katika utulivu imara wa mafakirio ya mengi katika ujenzi wa Taifa. (Kazi)

Na hii ni katika maana kubwa na kazi kubwa ya muziki, kwa maana muziki huleta faraja lakini hamasa ya ufanyaji kazi. (Haswa)

Achilio la tatu kwa mpigo kutoka kwa Darassa si kitu kidogo ukizingatia ushiriki wa Maua Sama pamoja na Jux. (Uwepo)

Ni wazi “mwenye sifa yake mpe” Darassa amefanya jambo kubwa kuachia tatu kwa mpigo ambapo ni wapi sasa usimsikie? (Hakuna)

Lakini nyimbo zote ni zenye ujazo kamili kuanzia audio mpaka video. (Abba-Hanscana) Hakika wanastahili pongezi. (Hongereni)

Sisi hatuna chaguzi katika hizi bali kuongeza katika orodha ya nyimbo zetu katika usikivu huku tukiendelea na maandiko. (Muziki)

Kwako ni ipi pendwa katika hizi tatu za Darassa? (Ulizo)

Leo Feat Jux

Tumepoteza Feat Maua Sama

Relax

Tuambie….

#MuzikiNiSisi