Darasaa bila hovyo na yupo ndani ya Zantel. (Naam)

Darassa bila hovyo na yupo ndani ya Zantel. (Naam)

Njia za Darasa ni za upekee mno, na hakika ni zenye mvuto imara mbele ya wajuzi wa muziki na mashabiki walio na utashi kamili. (Naam)

Hana hovyo hana kelele bali muziki wake katika upana. Huyu ni msanii Darasa tangia awali yake ya Sikati tamaa na Ben Paul mpaka Leo yake na Jux. (Muziki)

Huku wasanii wengine wengi wakipumbazwa na neno “Muziki Biashara” na wakiendelea kutafuta trend za mtandaoni Darasa yukimya na kuendelea na kazi yake ya muziki. (Uhalali)

Wasanii wengi hudhani “Muziki Biashara” ni kutrend katika mitandao ya kijamii kwa hovyo kuu. (Sikitiko)

“Muziki Biashara” ni upana wa utambuzi wa namna ya kutengenza chapa yako katika mauzo ya soko la muziki kwa kazi bora lakini taswira yako hata nje ya soko la muziki. (Makampuni)

Na kabla ya Kampuni kumtumia msanii tazamo kuu huwa Je! msanii huyu anatabirika? Hana badiliko la papo kwa hapo? (Ufahamu)

Maana wapo wasanii unaweza mpa ubalozi leo wa kampuni kisha kesho ni matendo makuu ya hovyo yenye kuchafua hata kampuni ambayo imempa ubalozi. (Soni)

Vivyo wale wasanii wenye hovyo za kutosha ni wazi kutumika na makampuni kwao itabaki kuwa ni habari ya kusimulia na kuona kwa wengine. (Naam)

Darasa hana pupa wala kupenda matukio ya hovyo bali muziki, nidhamu kuu na hata kutabirika katika kesho yenye utulivu. (Hakika)

Hongera kuu Darasa kwa kuwa balazi wa mtandao wa simu wa Zanteli (MsakoTime) ni jambo kuu na lenye maana katika kuamsha wasanii wathamini sanaa zao zaidi. (Pongezi)

Na hata mswahili hunena yakuwa “Mwenye pupa hadiriki kula tamu” Wenye hovyo za mitandaoni mtaendelea kula fedheha tu. (Chekesho)

#ZimaKikiWashaMuziki #MuzikiNiSisi #TuzungumzeMuziki