Cpwaa na juzi yenye ujazo, jana yenye ubora na sasa katika deni.

Cpwaa na juzi yenye ujazo, jana yenye ubora na sasa katika deni.

Mjuzi yupi wa muziki ambaye hajui upana wa Cp au Cpwaa katika ujazo kamili wa upana wa muziki?. Hakika hayupo na hatakaa atokee.

Juzi ya Cp ilikuwa ni katika ujazo kamili hakina hatuwezi kusahau kumbukumbu za Aisha Aisha, Nafasi nyingine, Semeni Ooh na nyingine nyingi.

Ujazo huu uliambatana na upana wa mwenzake ambaye ni Suma Lee ambapo kwa pamoja waliunda Parklane.

Lakini jana ya Cp yenye ubora ni katika Nimeshazoea, Six in the morning, So pwaa, Revenge, Chereko, Problem na Action hakika ni ubora wa uimbaji na uchanaji katika nyakati mosi.

Ni wasanii wachache mno wenye uwezo wa yote kwa usawa wa usawia na hatusiti kunena yakuwa Cp ni miongoni mwao.

Sasa yake ni katika ukimya mpana mno, ambapo sisi hatujui hasa ni mkwamo wake kwa maana ya katika ladha ya muziki ni msanii ambaye alikuwa mbele ya muda kwa upana mkubwa mno.

Ni wazi usasa wake umejaa deni kubwa kwa mashabiki wa kizazi cha mtandao yapasa wamsikie vyema maana uwezo wake ni mkubwa katika yote ya sasa yenye kuhusu muziki.

Muziki unamuhitaji vyema Cp hivyo hakuna kitakiwacho kwake zaidi ya kwenda kasi na hali ya muziki ulivyo ili aweze kulipa deni vyema kwa mashabiki wengi wa sasa.

#TuzungumzeMuziki