“Chid Benz uzuri wa godoro nje , ila kwa ndani mna pamba”

“Chid Benz uzuri wa godoro nje , ila kwa ndani mna pamba”

Tukisema ni “sikio la kufa” hakika hatupaswi kukosolewa kwa maana ya yeye alivyoeleza aliyopitia na hakutaka tena yajirudie katika maisha yake.

Kwa maelezo yake wakati anatumbulisha wimbo wake ambao amemshirikisha Q Chilla aliongea kwa ujasiri kiasi cha Team Tizneez kuandika andiko hili “Nguvu iliyotumika kusema mabaya ya Chid Benz, itumike tena kusema mazuri yake sasa”

Hii yote ilikuja katika kuona ni jambo jema kuunga mkono kazi zake kwa maana mapito yake ni yenye masikitiko lakini tunapaswa kujali na kuheshimu kipaji chake ambacho bado kina hitajika katika uwanja huu wa muziki wa kizazi kipya.

Lakini hakika Chid Benz ni nazi iliyoliwa na mwezi, kwa maana ya kukosa thamani mbele ya jamii.

Hakuna wa kumsaidia bali yeye mwenye kujisaidia, maana raha apatayo katika jambo la dawa za kulevya hatujui, wakati ukiwaza kumsaidia yeye anawaza namna ya raha apatayo katika jambo lake hilo zuri ambalo ni baya kwenye jamii.

Yapasa jamii ijue “Vita ya fimbo haiamuliwi kwa panga”. Nguvu watumiayo mashabiki,wachambuzi na hata Media katika kulaumu na kutoa lugha kali kwenye ukurasa wake wa ‘Instagram’ na kwingineko ni wazi haina maana yoyote ile. Bali yeye kuamua maisha mapya tofauti na aishiyo.

Lakini jamii yapasa ijue yakuwa “Pofu hasahau mkongojo wake” ila pia “Ng’ombe akivunjika guu hurejea zizini”

Hivyo kuna kila sababu ya Chid Benz kurudi tena katika nyumba za kupambana na kuzuia matumizi ya dawa za kulevya katika kuweka sawa tatizo lake hili. Kusiwe na haraka ya kutoka huko kwa maana ni wazi yaonekana tatizo lake ni kubwa.

Maana huenda yakawa haya haya ya “uzuri wa godoro nje ila ndani mna pamba” Kwa maana wengi humjaji kwa muonekano wa nje bila kujua ndani bado hamna uzuri huo.

Lakini “mzoea punda hapandi farasi”

hizi.

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Tuachie maoni yako hapa