Chid Benz amka na ujitazame kwenye kioo cha Lord Eyez

Chid Benz amka na ujitazame kwenye kioo cha Lord Eyez .

Kuzungumza kwa upana wa mifano yenye uhalisi wa uhalisia ni jambo jema na lenye kheri nyingi zaidi.

Nani mfuasi wa muziki wa hiphop na asijue wala kukumbuka nyakati mbaya za Lord Eyez?. Hakika hayupo.

Haikuwa rahisi katika mapito yake ambapo haikuwa kazi ngumu kwake kuweka mapito yake katika wimbo wake wa ‘Mapito’ akiwa na Damian Soul.

ingawaje nyakati fupi mbele jahazi lilizama tena, mapambano ya uokoaji yalikuwa mengi lakini wapi.

Lakini sasa nyakati zimekubali na ameweza kurudi katika uhalisi wake. Ikumbukwe Dunia aishio Chid Benz ndiyo Dunia ambayo pia Lord Eyez ameishi kwa nyakati nyingi. (Uhalisia)

Na hawa wote ni wasanii pendwa kwa mashabiki kwa upana wa kuwa na kazi ama kutokuwa nazo, hakika upendo wa mashabiki kwao hubaki na ujazo ule ule.

Na tunaona sasa Lord Eyez ametoka kwenye Dunia mbaya na amekuwa ni mpana katika kazi zake. Lakini muonekano wake ni wenye nuru yenye mng’ao ang’avu ambapo hakika inaleta tumaini jema.

Hivyo ni vyema Chid Benz akaamka kutoka kwenye Dunia mbaya ambapo ndipo alipolala na ajitazame katika kioo cha Lord Eyez na ajione yeye.

Maana upande huu wenye wema kwenye muziki ni upande kamili ambao ni wazi unahitajika zaidi.

Na wala tusichoke katika elekezo la Chid Benz katika uelekeo wenye maana zaidi, kwani daima “Pazeni sauti zenu katika ukombozi”

#TuzungumzeMuziki