“Chema hakikai, hakina maisha” Je! The Mafik wataishi nje ya semi hii?

“Chema hakikai, hakina maisha” Je! The Mafik wataishi nje ya semi hii?

Nani mpenda muziki na mjuzi asiyejua upana na ukubwa wao katika uimbaji? hakika hayupo.

Tungo, uimbaji, na kila mmoja kuwa na ladha yake kumefanya kila sikio liweze kusikia vyema ubora wao.

Lakini hofu yetu ni katika endelezo jema la kazi zao, maana historia inatuonyesha yakuwa wasanii wengi ambao walikuja katika hali ya muunganiko waliishia njiani na kila mmoja kushika njia yake.

Lakini yote ni kutokana na wahusika kutokujipanga tangu kuanza mwanzo, yani kufanya kazi katika ushikaji ushikaji zaidi, si makaratasi katika upana wake.

Hivyo ni vyema The Mafix kujitazama mapema katika makaratasi ili tuweze kuwa nanyi nyakati zote katika usikivu wa nyimbo nzuri na ladha tofauti.

Na ni vyema viongozi wajue yakuwa chanzo kikuu cha kubomoka kwa makundi ni mgawanyo wa maslahi, yafaa kila mmoja apate kipande stahiki sio mmoja viwili mwingine kimoja, hakika hapo mwisho utafika tena kwa chuki mbaya baina yao/yenu.

Na kama tunaamini muziki ni kazi basi ni vyema kuzifanya katika mikataba sio ubro ubro ambao mwisho wake huwa ni kutupiana lawama na maneno ya fedheha.

Naam! “tuthamini huu muda kabla haujageuka historia, kaka yetu Fid Q hunena semi hii nyakati zote na ni semi yenye uhalisi wa uhalisia.

#TuzungumzeMuziki