Chege ndiyo mwamba imara uliobaki kwa Said Fella

Chege ndiyo mwamba imara uliobaki kwa Said Fella

NA JOHN SIMWANZA

“Chege ndio mwamba imara Uliobaki kwa Fella“ Hiyo ni kauli yangu   na ndiyo ukweli ambao unazunguka kwenye mawazo ya wadau na mashabiki mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya kwa sasa.

Kauli hii inakuja kutokana na hali halisi iliyopo kwa muda sasa katika kundi la Wanaume family lililochini ya Said Fella.

Kabla na hata baada ya kugawanyika kwa kundi hili la Wanaume family Chege Chigunga amekuwa sio msanii wa kukifunga kinywa chake kama  ilivyo kwa Wasanii wengine ambao walikua katika kundi moja. Japo nyimbo za kundi zilikua zinatoka mara kwa mara lakini Chege bado alikuwa anaibuka katika kazi zake binafsi na kumfanya awe na mashabiki tofauti ndani na nje ya kundi.

Kuna baadhi ya makundi ambayo yamekwisha vunjika na yalikuwa na ukubwa kama kundi la Wanaume family. Hivyo kutokuwepo kwa Wanaume family kwa sasa hiyo hainishangazi kwa maana muziki ndivyo ulivyo.

Kwakuwa tumewaona wasanii wengi ambao walikuwa kwenye kundi wanapotea mara baada tu ya kutetereka kwa kundi au kuvunjika lakini Chege ameonekana kuitetea nafasi yake Zaidi hasa katika kipindi hiki ambacho kundi halisikiki kama zamani.

Lawama za mameneja juu ya kupishana na wasanii wanaokuwa wanawasimamia au msanii kuulalamikia uongozi ambao unamsimamia jambo hilo limekuwa nila kawaida. Lakini kwa upande wa Chege na Fella hawajawahi  kufikia katika hatua hiyo yakuweka matatizo yao kwa mashabiki hali hiyo inaashiria kushibana na kuwa na uelewano mkubwa katika maisha yao ya kazi na nje ya kazi.

Kutokana na kukaa kwa muda mrefu katika uongozi wa Said Fella, Chege anakila sababu ya kumfanya Fella ajivunie kuwa ni kiongozi bora wa wasanii japo kuna baadhi ya wasanii ambao wamepita kwa na kukaa kwa kipindi kifupi katika mikono ya Fella lakini hiyo haimfanyi Mkubwa Fella akashindwa kujivunia kwa mtoto wa mama said Chege chigunda.

Huu ni moja kati ya mifano mizuri katika muziki wa kizazi kipya, lakini tunaamini haya yote yameletwa na nidhamu ya Sanaa juu ya Chege kwenda kwa meneja wake. “Baniani mbaya kiatu chake dawa”

Follow Twitter Tizneez

Facebook page Tizneez

Instagram Tizneez

Youtube Tizneez

Tuachie maoni yako hapa