CHANGAMOTO YA WASANII KUHIFADHI KAZI ZAO

Tafakari ya leo imenifanya nifike hapa kwenye hili swala ambalo kwa kiasi fulani limenisikitisha na kunishangaza. Niliwahi kumuomba msanii mmoja wa Bongo Fleva wimbo wake ambao waliufanya miaka ya nyuma. Kilichonishangaza na kunisikikitisha ni jibu la msanii huyo kwamba hana wimbo wake huo ambao uliwahi kufanya vizuri kipindi cha nyuma. SIkuishia hapo nikajaribu kufanya utafiti mfupi kwa baadhi ya wasanii wa zamani lakini wengi wao walionyesha kutokuwa na nyimbo zao za zamani.

Azure

Microsoft Azure inakuwezesha kuhifadhi data zako zote mtandaoni kwa kipindi chote zikiwa salama.

 

Hii pia ndio sababu kubwa iliyoipelekea Microsoft kutengeneza Microsoft Azure, hii ni cloud server ambayo inakuwezesha licha ya kuhifadhi data zako kwenye cloud ambazo utakuwa na uhakika wa kuzipata lakini pia inakuwezesha kuhost website yako au hata database. Hii ndio tofauti kuu kati ya Microsoft Azure na Cloud Server nyingine. Nyingi ya server hizi ni kwamba zinamuwesha tu kuhifadhi tu vit vyake kama video, sauti, picha na documents.

Office 365

Microsoft Office 365 itakuunganisha na kila mtu katika kufanya kazi. Ni rahisi na nafuu.

 

Lakini Microsoft hawakuishia katika server tu. Kwa kutambua uhuru wa mtu, wametulea program ya Office 365, program ambayo inakuondoa katika utumwa wa kukaa mbele ya dawati lako la kazi kila siku na wakati wote. Kupitia program hii unaweza kufanya kazi ukiwa mahali popote, sio lazima uwepo ofisini.

Kuna haja ya wasanii wetu kujifunza namna ya kuhifadhi kutunza mziki wao kwa kutumia teknolojia kama Microsoft Azure. Hii itafanya wawe na uwezo wa kuhifadhi nyimbo zao kwa muda mrefu zaidi na kwa usalama thabiti. #DoMore

Soma: JINSI TEKNOLOJIA ILIVYOPIGA TAFU MZIKI WETU