Chaguzi la Nikki Mbishi na Wakazi ni sahihi kwa Castle Lite.

Chaguzi la Nikki Mbishi na Wakazi ni sahihi kwa Castle Lite.

Ni mtu pekee asiyejua upana wa hiphop Tanzania na ataje wasanii wakubwa wa hiphop bila tajo la Wakazi na Nikki Mbishi. Bali wenye ujuzi hakika mabingwa ni Wakazi na Nikki Mbishi. (Iko Wazi)

Tunapozungumzia wasanii bora  kwenye hiphop tunatazama wasanii wenye ujazo wa album na kanda mseto, lakini ushawishi imara katika wasanii wengine wachanga wa hiphop. (Nikki Mbishi-Wakazi)

Tukitazama nguvu ya ushawishi juu ya Wakazi na Nikki Mbishi katika uhalisi wa Hiphop ni kubwa mno na hii ni kuanzia mtandaoni mpaka maisha ya kawaida. Na hili limejidhihilisha vyema katika upana wa mwaamko wa Chalenji ya #NabebwaNaBeatChallenge na #CastleLiteUnloks. (2019)

Ambapo mpaka sasa Chalenji hii imepata washiriki wengi mno. Ambapo kuanzia mtandao wa Twitter na Instagram tumeona namna jinsi ambayo chalenji hii ikitrend vyema. (Mafanikio)

Imefanikiwa hivi kwa ukubwa wa hiphop yenye uhalisi kati ya Nikki Mbishi na Wakazi. Hakika hii inatufanya tupongeze Castle Lite kwa kuona na kujua uhalisi wa hiphop kwa chaguzi sahihi la Nikki Mbishi na Wakazi. (Pongezi)

Hakika tunahitaji kuona wadau wakitumia watu sahihi kulingana na jambo husika, ingekuwa ni kichekesho kikubwa kuwakilisha hiphop Tanzania na kutowatumia wasanii kama Wakazi na Nikki Mbishi. (Kabisa)

Pia pongezi kwa wasanii wote ambao wameshiriki katika na kuonyesha uwezo hakika inaleta hamasa kwa namna ya kila mmoja kuja na upana wa mitambao na mistari yenye jazo kamili. (Muziki)

Hakika Hiphop iko katika mstari kamili wenye unyoofu imara, lakini daima “Kweli haishindwi hata siku”. (Naam)

#MuzikiNiSisi